Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkenya, Mkongo wapishana Pamba

MKONGO

Muktasari:

  • Mwaku aliyejiunga na Singida Agosti 5, 2025, akitokea FC Saint-Eloi Lupopo ya kwao DR Congo, amekamilisha usajili huo wa kujiunga na Pamba, huku Mwanaspoti likitambua nyota huyo amejiunga na timu hiyo kwa mkopo na sio kuuzwa moja kwa moja.

MABOSI wa Singida Black Stars wamefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Pamba Jiji, Mkenya Mathew Tegisi Momanyi, baada ya kuridhishwa na kiwango chake alichokionyesha Ligi Kuu Bara kwa kufunga mabao 11, msimu wa 2025-2026.

Wakati hilo likikamilika, uongozi wa Pamba Jiji umefikia makubaliano na Singida ya kumsajili mshambuliaji wa kikosi hicho Mkongomani Malanga Horso Mwaku baada ya nyota huyo kuifungia timu hiyo mabao manne ya Ligi Kuu msimu wa 2025-2026.

Mwaku aliyejiunga na Singida Agosti 5, 2025, akitokea FC Saint-Eloi Lupopo ya kwao DR Congo, amekamilisha usajili huo wa kujiunga na Pamba, huku Mwanaspoti likitambua nyota huyo amejiunga na timu hiyo kwa mkopo na sio kuuzwa moja kwa moja.

Chanzo kutoka timu hiyo, kiLIliambia Mwanaspoti Mwaku ametolewa kwa mkopo kwa ajili ya kupata nafasi ya kucheza zaidi, hasa baada ya Singida kumrejesha mshambuliaji, Jonathan Sowah aliyekuwa anaichezea Simba msimu wa 2025-2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Pamba, Ezekiel Ntibikeha, amesema kuna mazungumzo yanaendelea na nyota mbalimbali ili kupata saini zao, baada ya kupokea ripoti ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Mkenya Francis Baraza.

“Baada ya kupokea ripoti ya benchi la ufundi tayari uongozi tumeanza kuifanyia kazi na wapo wachezaji mbalimbali ambao muda wowote tutakamilisha sajili zao, mchakato huu tulianza mapema na tuko katika hatua nzuri zaidi,” amesema Ntibikeha.

Mwanaspoti linatambua wakati Pamba Jiji ikimnasa Malanga Horso Mwaku, wachezaji wengine waliotoka timu hiyo na kwenda kujiunga na Singida ni kipa, Yona Amos, kiungo mkabaji, James Mwashinga na mshambuliaji raia wa Kenya, Mathew Tegisi Momanyi.