Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zahera amtega Ajibu Coastal Union

WAANDISHI WETU


WAGOSI wa Kaya, Coastal Union inaendelea kujifua kujiandaa na Ligi Kuu Bara inayoanza kesho, huku kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera akimtega Ibrahim Ajibu akitaka kumpa unahodha kama alivyofanya walipokuwa Yanga misimu mitano iliyopita.

Uamuzi huo umeelezwa kuwashtua baadhi ya wanamangushi kutokana na ukweli Ajibu ni mgeni katika kikosi hicho, lakini Zahera alisema nyota huyo wa zamani wa Simba, Yanga, Azam na Singida Big Stars ana vitu vinavyombeba kupewa kitambaa.

Ajibu (26), amekuwa akifanya makubwa uwanjani kwa ujuzi wa  kumiliki mpira, kupiga pasi za mwisho za mabao ya kideoni,  lakini ameshindwa kuwa kwenye kiwango tangu alipoachana na Zahera na kurejea Msimbazi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Zahera alisema “Ibrahim Ajibu ana mchanganyiko wa vitu vingi ikiwemo talanta (kipaji), kujitolea na ukomavu wa miaka mingi. Ameonyesha sifa za uongozi na anafaa, pia naamini ni wakati wa kuonyesha uwezo wake akiwa kama nahodha,” alisema Zahera.

Ajibu mwenyewe alipoulizwa juu ya tarifa za kupewa tena kitambaa, alishukuru kwa kusema; “Ni heshima kubwa ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa wenzako na mtetezi wao. Nimekuwa nikijitahidi kuongoza kwa kuonesha mchango mzuri wa mafanikio ya timu. Ikiwa nimepewa fursa, nitafanya kazi nzuri ya kuhamasisha wenzangu na kuwaongoza kwa ushindi.”

Hata hivyo, Ajibu atalazimika kufanya kazi ya ziada kwani tangu alipoondoka Yanga mwaka 2019, hajarejea kwenye makali yake na kupewa kitambaa hicho kwake itakuwa ni kama mtego ambao lazima autegue kutuliza nyoyo za Wana mangushi walioanza minong’ono mapema kutokana na sifa za uvivu zinazodaiwa kuwa nazo kiungo huyo mshambuliaji.

Katika hatua nyingine, timu hiyo imeendelea kufanya usajili ikiwa mbioni kumalizana na mshambuliaji Mkongo, Henock Mayala, aliyekuwa akikipiga Polisi Tanzania iliyoshuka daraja msimu uliopita sambamba na Ruvu Shooting na Mbeya City.

Mbali na Mayala, pia Coastal imemalizana na Mcrotia Fran Golubic aliyepewa mkataba wa miaka miwili, siku chache baada ya kugoma  alipotakiwa kufanya majaribio.

“Tunamalizia malizia kusajili sasa, kwa wachezaji wa ndani ambaye bado hajasaini ni Mapinduzi Balama ingawa tumefanya naye mazungumzo tayari,” kilisema chanzo hicho.

Coastal hadi sasa imesaini wachezaji sita akiwamo Ibrahim Ajibu, Ally Kombo (Ruvu Shooting), Lucas Kikoti (Namungo), Abdallah Denis (Malindi), Dennis Modzaka (Bechem United), Abdulswamad Kassim (Geita Gold).