Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yatambulisha jezi ya miaka 90

Muktasari:

  • Tofauti na miaka kadhaa nyuma mashabiki wa Simba wameonekana kuipokea jezi hiyo vizuri kutokana na ubora ambao umeonyeshwa na kampuni ya Diadora ambayo ndiyo imefanya dizaini.

KLABU ya Simba jana ilitambulisha jezi mpya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, huku mzabuni wa jezi hizo Joseph Rwegasira akisema uzi huo umezingatia klabu hiyo kusherehekea miaka 90 tangu kuanzishwa kwake.

Tofauti na miaka kadhaa nyuma mashabiki wa Simba wameonekana kuipokea jezi hiyo vizuri kutokana na ubora ambao umeonyeshwa na kampuni ya Diadora ambayo ndiyo imefanya dizaini.

Jezi hizo zina rangi ambazo zimekuwa zikitumiwa na klabu hiyo ambazo ni nyekundu, nyeupe na buluu huku beki mahiri wa timu hiyo, Rushine de Reuck akitumika kwenye uatambulisho huo rasmi wa klabu.

Jezi za nyumbani zitakuwa na rangi nyekundu, nyeupe zitatumika kwa mechi za ugenini na jezi ya rangi ya bluu itakuwa ya tatu.

Uzinduzi rasmi wa jezi za Simba unafanyika rasmi jana Jumamosi, Agosti Mosi, 2026 mkoani Arusha katika Hifadhi ya Ngorongoro ambapo klabu hiyo ilitangaza wiki nzima kuwa itakwenda kufanyia huko uzinduzi huo.

“Kila kitu kwenye jezi hii kimezingatia ubora, pamoja na mambo men gine mengi lakini kwenye dizaini na mambo mengine yalikuwa chini ya Diadora lakini tumekuwa tukishirikiana pamoja haswa ukizingatia mwaka huu klabu inatimiza miaka 90 tangu kuanzishwa kwake, jezi zetu zimezingatia ujumbe wa miaka 90, tunatarajia kurudisha ufalme wetu kwenye jezi, nyikani ndiyo maana tumeenda Ngorongoro lakini pia tunatarajia kurudisha ufalme wetu uwanjani,” alisema Rwegasira maarufu kama Jayrutty.

 Hii imekuwa timu ya kwanza nchini kutambulisha jezi zake kwa ajili ya msimu ujao, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kubwa pia jezi za klabu ya Yanga ambayo kwa hivi karibuni imekuwa na ufalme wake kwenye uzi wa msimu.