Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga unbeaten.....

Yanga unbeaten.....

Muktasari:

NANI wa kuizuilia Yanga? Ni kauli za kejeli zilizotolewa na baadhi ya mashabiki ya Yanga zikisindikizwa na mabango kadhaa ya kufagilia chama lao ambalo jana liliendelea kugawa dozi nyingine katika Ligi Kuu Bara, ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo mpaka sasa.

NANI wa kuizuilia Yanga? Ni kauli za kejeli zilizotolewa na baadhi ya mashabiki ya Yanga zikisindikizwa na mabango kadhaa ya kufagilia chama lao ambalo jana liliendelea kugawa dozi nyingine katika Ligi Kuu Bara, ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo mpaka sasa.

Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-0 ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya huku nyota wao mpya, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ akiendelea kufanya yake uwanjani.

Ushindi wa Yanga ulikuwa ni wa 13 msimu huu katika mechi zao 17 na kuifanya imalize duru la kwanza ikifikisha pointi 43, pia ikihitimisha siku 286 ikicheza michezo 29 ya ligi bila kupoteza mchezo wowote. Siku hizo ni sawa na saa 6,864 au dakika 411,840. Kama hujui ni kwamba mara ya mwisho kwa Yanga kupoteza mchezo katika ligi ilikuwa Machi 12, mwaka huu walipolala 1-0 mbele ya KMC na baada ya hapo imecheza michezo hiyo ukiwamo wa jana bila kupoteza huku ikikusanya pointi 65 kwa kushinda michezo 18 na kupata sare 11, ikifunga mabao 43 na kuruhusu nyavu zao kuguswa mara 15 tu.

Katika mchezo wa jana, Kocha Cedric Kaze aliamua kumuanzisha Saido na kumtupa benchi Michael Sarpong kutoka kikosi kilichocheza na Dodoma Jiji na kuifumua pia mabao 3-0 kwenye mchezo wao uliopita uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kuanza kwa Saido kuliendelea kuwapa raha mashabiki kwani jamaa licha ya kutofunga bao, lakini alitengeneza mabao mawili yaliyofungwa na Deus Kaseke na Yacouba Songne na kumfanya mshambuliaji huyo kutoka Burundi kuhusika na mabao manne, akifunga moja na kuasisti matatu mpaka sasa. Saido pia alifunga mabao mawili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United, ulioisha kwa Yanga kushinda mabao 3-0 mjini Singida wiki iliyopita.

MCHEZO ULIVYOKUWA

Ihefu ndio iliyouanza mchezo huo kibabe ikifanya shambulizi kali dakika ya saba ya mchezo ambapo winga wao mpya Juma Mahadhi anayewatumikia kwa mkopo akitokea Yanga aliachia shuti kali lililopanguliwa Metacha Mnata na mpira kumkuta Joseph Mahundi, lakini pasi yake kwa Joseph Kinyozi ikikosa macho.

Yanga ilijibu mapigo dakika ya 12 kwa Saido anayemfukuzian Clatous Chama katika kuasisti mabao akimpenyezea pasi tamu Kaseke, ambaye hakufanya kosa kwa kuukwamisha wavuni kuandika bao lake la nne msimu huu na la kwanza katika pambano hilo.

Yanga waliendelea kutulia na kufanya mashambulizi makali lango la Ihefu lakini uimara wa kipa Deogratias Munishi ‘Dida’ dakika ya 18 uliinusuru timu yake kupigwa bao la pili kupitia kichwa safi cha mshambuliaji Yacouba Sogne na kuudaka kiufundi mpira huo.

Dida alisajiliwa na Ihefu katika dirisha hili dogo la usajili ambapo katika mchezo wa jana alionekana kuwasaidia akicheza vyema mipira ya adhabu na krosi za Yanga katika mchezo huo.

Dakika ya 32 Kinyozi tena almanusura aisazishie timu yake lakini anapiga shuti hafifu akipokea pasi ya Jeremia Katula wakati Ihefu wakitengeneza shambulizi zuri na dakika 10 baadaye Yanga nusura ipate baada ya kazi nzuri ya winga Tuisila aliyegongeana vyema na Songne mpira ukamkuta Feisal Salum lakini shuti lake linawagonga mabeki wa Ihefu na wenyeji kusalimika.

Ihefu ilifanya mabadiliko dakika mbili kabla ya mapumziko kwa kumtoa Jeremia Katula nafasi yake ikichukuliwa na Willy Mgaya yakiwa ni mabadiliko ya ufundi katika kuboresha safu yao ya kiungo.

Hata hivyo dakika nne baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Yanga walishtukiza tena wenyeji wao kwa kuandika bao la pili lililowekwa kimiani na Songne akipokea pasi murua ya Saido aliyetengua mtego wa kuotea wa mabeki wa Ihefu na kumpiga chenga kipa Dida.

Kocha Kaze aliamua kumtoa Mukoko Tonombe nafasi yake ikichukuliwa na kiungo mwingine mkabaji Zawadi Mauya kabla ya Saido kumpisha Farid Mussa mabadiliko yaliyozidi kuinufaisha Yanga kwani dakika ya 60, iliandika bao la tatu lililowekwa kimiani na Feisal Salum kwa shuti hafifu akimalizia pasi ya Kaseke. Ihefu ilimtoa Mahadhi na kumuingiza Andrew Simchimba aliyetua klabu hapo kwa mkopo kutoka Azam aliyeichangamsha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo akishirikiana na kinara wao wa mabao, Joseph Kinyozi.

Ihefu walionekana kuzinduka na kutaka kutafuta bao la kufutia machozi ambapo dakika ya 62 Simchimba alipoteza nafasi nzuri shuti lake kali lilipanguliwa na Mnata na kuutema mpira kisha kuuwahi na kuudaka tena.

Dakika ya 74 Kinyozi tena alikosa utulivu akiinyima timu yake bao shuti lake kali akiwa karibu na Mnata linadakwa vyema akiipotezea timu yake nafasi nyingine nzuri.

Yanga walifanya mabadiliko mengine dakika ya 76 wakimtoa Kaseke aliyetengeneza bao la tatu nafasi yake kuchukuliwa na Haruna Niyonzima yakiwa ni ya kutuliza eneo la kiungo na mpaka dakika 90 zilipomalizika matokeo yalikuwa 3-0