Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Simba kujua wapinzani CAF Agosti 6, bingwa kuondoka mabilioni

Muktasari:

  • Droo hizo zitazipa klabu kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika nafasi ya kufahamu wapinzani wao wa kwanza katika harakati za kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya mashindano hayo mawili makubwa ya CAF.

CAIRO, Misri: SAFARI ya kuwania ubingwa wa mashindano ya klabu barani Afrika kwa msimu wa 2026/27 itaanza rasmi Alhamisi, Agosti 6, wakati Shirikisho la Soka Afrika (CAF) litakapofanya droo ya hatua za awali za Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika jijini Cairo, Misri.

Droo hizo zitazipa klabu kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika nafasi ya kufahamu wapinzani wao wa kwanza katika harakati za kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya mashindano hayo mawili makubwa ya CAF.

Vigogo wa Tanzania, Yanga na Simba zinasubiri kwa hamu kujua wapinzania wao katika Ligi ya Mabingwa huku katika Kombe la Shirikisho, Azam na Singida Black Stars watapeperusha bendera huko.

Msimu uliopita klabu hizo za Tanzania ziliweka rekodi kwa zote kufuzu kwa hatua ya makundi japokuwa hakuna hata moja iliyovuka hatua hiyo.

Hafla hiyo itaanza na upangaji wa ratiba ya Kombe la Shirikisho saa 14:00 kwa saa za Cairo (sawa na saa 9:00 alasiri kwa saa za Tanzania), ikifuatiwa na kura ya Ligi ya Mabingwa saa 15:00 kwa saa za Cairo (sawa na saa 10:00 jioni kwa saa za Tanzania).

Sherehe zote mbili zitarushwa mubashara kupitia CAF TV, zikiwapa mashabiki wa soka barani Afrika na duniani kote fursa ya kushuhudia mwanzo wa msimu mpya wa mashindano ya klabu.

Mbali na heshima ya kutwaa ubingwa wa Afrika, CAF imeendelea kuongeza motisha kupitia zawadi nono za fedha.

Bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika ataondoka na kitita cha Dola 6 milioni,(sawa na zaidi ya Sh16 bilioni za Tanzania, huku bingwa wa Kombe la Shirikisho akijinyakulia Dola milioni 4, (sawa na zaidi ya Sh10.8 bilioni.

Aidha, klabu zote zitakazoishia kutolewa katika hatua za awali zitapatiwa kifuta jasho cha Dola 100,000 (zaidi ya Sh270 milioni) ikiwa ni sehemu ya mpango wa CAF wa kusaidia maendeleo ya klabu zinavyoshiriki mashindano hayo.

Katika misimu ya hivi karibuni, hatua za awali zimekuwa zikitengeneza mechi zenye ushindani mkubwa na matokeo ya kushtua, huku zikikutanisha vigogo wa soka la Afrika na klabu zinazochipukia zinazotafuta kuandika historia.

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wakati USM Alger ya Algeria ndiyo bingwa mtetezi wa Kombe la Shirikisho Afrika.