Yanga, Simba ulinzi kama wote kwa Mkapa

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi limejipanga vyema kiusalama kuelekea kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam Aprili 30 mwaka huu.
Akizungumzia na wanahabari leo Alhamisi 28, 2022 Kamanda huyo alisema wamejipanga kuimarisha ulinzi huo ndani na maeneo jirani kuhakikisha watu wote wanazingatia sheria na taratibu za mchezo wa soka katika kuingia na kutoka.
“Tunatambua mchezo unavuta hisia kali. Vitu vyote vinavyohusiana na silaha za moto na zisizo silaha za moto ikiwemo visu, mapanga,chupa makopo havitaruhusiwa kuingizwa au kuwekwa sehemu za mashabiki,”alisema
Amesema wanaweka usalama huo kwakutambua uzito kutokana na utani uliopo kwa timu hizo hivyo wamejipanga kuona wote wanaangalia mechi kati mazingira salama.
Amesema Jeshi hilo halitakuwa na msamaha kwa mtu yeyote atakayeonekana kujihusisha na vitendo vya vurugu au kikundi huku akiwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa fiche za kiarifu na kwamba jeshi hilo litatunza siri na kuwashughulikia watakaokuwa na nia hiyo.