Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yashusha watatu akiwemo kipa

YANGA Pict

Muktasari:

  • Wananchi hao wa kike wanaonekana kubadili mwelekeo na kuanza kuwekeza zaidi kwenye damu changa zenye uwezo wa kukua na kuwa sehemu ya muda mrefu ya kikosi hicho.

NI wazi kuna kitu kimebadilika kwenye usajili wa Yanga Princess msimu huu. Ndiyo, kutokana na tetesi za usajili zinazodaiwa kumalizana na wachezaji kadhaa vijana.

Wananchi hao wa kike wanaonekana kubadili mwelekeo na kuanza kuwekeza zaidi kwenye damu changa zenye uwezo wa kukua na kuwa sehemu ya muda mrefu ya kikosi hicho.

Yanga inadaiwa kumalizana na wachezaji watatu vijana

ikiwamo kiungo mshambuliaji Semeni Juma, mshambuliaji Winfrida Charles na kipa Robi Daudi, wote wakisaini mikataba ya miaka miwili.

Semeni anajiunga na Yanga akitokea Bunda Queens ya Mara, huku usajili huo ukimpa nafasi ya kuanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka katika moja ya klabu zinazolenga kufanya vizuri katika ligi. Kiungo huyo mshambuliaji amekuwa miongoni mwa vipaji vilivyoibuliwa na Bunda Queens katika miaka ya hivi karibuni.

Kutoka Bunda Queens, anafuata nyayo za wachezaji wengine kama Ester Maseke anayekipiga JKT Queens na wengineo ambao wamepata nafasi ya kuonyesha uwezo wao katika klabu hiyo.

Mwingine ni Winfrida Charles anayetarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji, akitokea Fountain Gate Princess kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kuonyesha uwezo msimu uliopita.

Mbali na huyo kipa Robi Daudi amekamilisha uhamisho wake kutoka Alliance Girls na kusaini mkataba wa miaka miwili na Yanga Princess. Ujio wake unaongeza chaguo katika eneo la kipa ambalo linaongozwa na Rita Akarekor, huku akiwa miongoni mwa wachezaji vijana ambao klabu hiyo imeamua kuwapa nafasi katika mpango wake wa muda mrefu.

"Msimu huu imefanywa tamthmini ya wapi tumekosea, tumerekebisha, hatuzungumzi sana kwa sababu viongozi tumewekeza kwenye usajili wa wachezaji wa muda mrefu kwa hiyo niwaondoe hofu mashabiki wa Yanga Princess kuwa msimu huu tunaamini tutafanya vizuri zaidi ya uliopita," amesema Mratibu wa Yanga, Kibwana Matokeo.