Yanga jeuri, mabosi wagawana anga kibabe
Muktasari:
- Hapa KMC Yanga imekuwa na tafrija yake ikiujaza Uwanja wa huo kwenye tukio maalum la utambulisho wa kiungo wake Stephanie Aziz KI aliyerejea klabuni hapo.
Yanga imewanyika kwenye matukio mawili Leo na yote mazito lakini hatua hiyo imewagawanyisha mabosi wake kibabe wakiongoza mashambulizi.
Hapa KMC Yanga imekuwa na tafrija yake ikiujaza Uwanja wa huo kwenye tukio maalum la utambulisho wa kiungo wake Stephanie Aziz KI aliyerejea klabuni hapo.
Tukio hilo likaongozwa na Rais wa klabu hiyo injinia Hersi Said aliyemtambulisha kiungo huyo huku pia akimkabidhi jezi maalum yenye namba 10 atakayoitumia Azizi KI.
Namba hiyo itakumbukwa awali ilikuwa ikitumiwa na Azizi KI kabla ya kuuzwa Wydad Athletic ambapo baada ya kuondoka, akakabidhiwa Pacome Zouzoua.
Baada ya tukio hilo Hersi akaungana na mashabiki wa timu hiyo waliojaa Uwanja mzima wakifuatilia mchezo huo kwenye televisheni kubwa uwanjani hapo pamoja na viongozi wengine.
Wakati Hersi akiwa KMC Makamu wake Arafat Haji naye akawa anga nyingine akiwa na kikosi hicho Mkoani Lindi kwenye mchezo wake wa kwanza msimu huu dhidi ya Namungo ya Lindi.
Arafat ameonekana jukwaani akiwa na simu yake huku akifuatilia tukio la utambulisho wa Aziz KI, huku akionyesha simu hiyo kwa mashabiki ambao wakati huo walikuwa wakiimba jina la mfadhili wao Ghalib Said Mohammed 'GSM' kwa kuita GSM GSM GSM.