Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuvunja mkataba wa Mbongo Ureno bilioni 200

MBONGO Pict

Muktasari:

  • Irakunda kiasili ni Mtanzania kwani alizaliwa Februari 9, 2006 katika kambi ya wakimbizi mkoani Kigoma ambako familia yake ilikimbilia ili kutafuta hifadhi kutokana na vita ya Burundi.

KOCHA wa Sporting CP ya Ureno, Rui Borges amesema mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich, Nestory Irankunda aliyezaliwa  Tanzania yupo nchini humo kukamilisha dili la kujiunga na timu hiyo.

Irakunda kiasili ni Mtanzania kwani alizaliwa Februari 9, 2006 katika kambi ya wakimbizi mkoani Kigoma ambako familia yake ilikimbilia ili kutafuta hifadhi kutokana na vita ya Burundi.

Kocha huyo amesema Irankunda ni mchezaji ambaye klabu hiyo ilikuwa inamhitaji kwa muda mrefu na inaamini ataongeza nguvu kwenye kikosi chake.

Nyota huyo anayeitumikia timu ya taifa ya Australia aliwasili Lisbon wiki iliyopita kwa ajili ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Watford ya England.

MBO 01

“Sitaki kusema uongo hapa, nadhani yuko huko akisaini sasa,”  amesema Borges huku akicheka, akieleza kuwa Irankunda ni mchezaji mwenye sifa tofauti na waliokuwa nazo kwenye kikosi chake.

Kocha huyo amesema ana hamu ya kufanya kazi na mshambuliaji huyo ili kuelewa zaidi uwezo wake na namna atakavyoweza kusaidia kuifanya Sporting kuwa timu yenye nguvu zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa, Irankunda anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano ambao atalipwa takribani Euro milioni 2.5 kwa mwaka, sawa na Sh 7.65 Bilioni za Kitanzania kwa mwaka.

Lakini zaidi ya mshahara huo, Sporting inadaiwa kuweka kifungu cha kuvunja mkataba cha euro milioni 80, kiasi ambacho ni takribani Sh244.8 bilioni.

Kwa thamani hiyo, klabu yoyote itakayomtaka Irankunda  italazimika kujiandaa na kiasi kikubwa cha fedha iwapo kifungu hicho kitakuwa sehemu ya mwisho ya mkataba wake.

MBO 02

Mshambuliaji huyo alianza kupata umaarufu mkubwa msimu wa 2023/24 aliposajiliwa akitokea Adelaide United akicheza mechi 25 za A-League na kufunga mabao nane huku akitoa asisti sita.

Kiwango hicho kiliwavutia mabosi wa Bayern Munich waliosajili kwenye timu ya vijana na baadae kupata mafunzo kwenye timu y wakubwa, ambako alifunga mabao manne katika mechi 15

Akiwa Bayern, Irankunda alipelekwa kwa mkopo Grasshopper ya Uswisi mwaka 2025, ambako alicheza mechi 21 za ligi, akafunga bao moja na kutoa asisti tatu. Baada ya hapo alihamia Watford, ambako msimu wa 2025/26 alionyesha uwezo mkubwa katika Championship kwa kucheza mechi 40, na kufunga mabao manne na kutoa asisti nne.