Suluhu Academy kutumika AFCON
Muktasari:
- Kauli hiyo ameitoa wakati wa zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa nyumba za maendeleo Kibuteni, Mkoa wa Kusini Unguja, kwenye Tamasha la Kizimkazi lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma, amesema Uwanja wa Suluhu Sports Academy ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa nyumba za maendeleo Kibuteni, Mkoa wa Kusini Unguja, kwenye Tamasha la Kizimkazi lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Amesema, wakaguzi wa viwanja vya AFCON watarajiwa kuwasili mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya kufanya ukaguzi kwa viwanja mbalimbali vitakavyotumika kwenye mashindano hayo.
“Uwanja huu uliopo Mkoa wa Kusini Unguja, unatarajiwa kuwa fursa muhimu kwa wananchi hususani wa maeneo ya Kizikimzaki, Makunduchi, Paje na maeneo mengine,” amesema.
Alieleza kuwa, kadiri ya mashindano hayo yanavyokaribia, ndivyo ambavyo Zanzibar inalenga kupata idadi kubwa ya wageni wakiwemo wachezaji mashuhuri, mashabiki na viongozi wa timu.