Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Pemba asisitiza jambo Kabaddi

KABADI Pict

Muktasari:

  • Pembe ameyasema hayo katika fainali ya Mashindano ya Afrika ya Kabaddi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Ndani wa New Amaan Complex, Zanzibar, ambapo Kenya iliibuka bingwa baada ya kuifunga Uganda kwa jumla ya pointi 31-21.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Riziki Pembe Juma, amesema mchezo wa Kabaddi una nafasi kubwa katika kuimarisha afya ya akili na mwili, akitaka jamii kuendelea kuutumia kama sehemu ya kujenga afya na ustawi wa wananchi.

Pembe ameyasema hayo katika fainali ya Mashindano ya Afrika ya Kabaddi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Ndani wa New Amaan Complex, Zanzibar, ambapo Kenya iliibuka bingwa baada ya kuifunga Uganda kwa jumla ya pointi 31-21.

Waziri huyo, amesema kutokana na umuhimu wa michezo katika afya ya mwili na akili, kuna haja ya kuongeza ushiriki wa makundi mbalimbali ya jamii katika michezo, akitoa wito wa kuwashirikisha hata wazee ili nao waweze kunufaika na shughuli za michezo kulingana na uwezo wao.

Amesema, Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa michezo katika kuhakikisha michezo mbalimbali inapata nafasi ya kukua na kuendelezwa Zanzibar.

Kwa upande wa Rais wa Shirikisho la Kabaddi Zanzibar, Abdalla Abeid Juma, amesema Zanzibar ni mwanachama mpya katika mchezo huo duniani na imeendelea kuongeza ushiriki wake katika mashindano ya kimataifa.

Amesema Zanzibar tayari imeshiriki mara nne katika mashindano ya dunia ya kabadi kwa wanawake, hatua inayoonesha kuwa mchezo huo unaendelea kupata nafasi nchini.

Abdalla amesema Mashindano ya Afrika yaliyofanyika Zanzibar yalitarajiwa kushirikisha nchi 15, lakini nchi saba ndizo zilizoweza kushiriki, huku akizipongeza nchi hizo kwa kuonyesha vipaji na ushindani katika mashindano hayo.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar, Said Kassim Marine, aliipongeza kamati ya maandalizi kwa kazi kubwa iliyofanya kufanikisha mashindano hayo.

Said amesema kuandaa mashindano ya Afrika si jambo dogo, hivyo mafanikio ya mashindano hayo yanaonyesha juhudi na ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kuendeleza michezo Zanzibar.