Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Warembo halafu wanajua kuimba

MUZIKI wa kizazi kipya nchini maarufu kama Bongo Fleva zamani ulikuwa na sauti chache katika upande wa wadada, hiyo ilitokana na jinsi ambavyo mziki ulivyokuwa unaenda ilikuwa ngumu kusikia tofauti na sauti za wadada ambao wamezoeleka.

Ilizoeleka kusikia sauti za Keisha, Ray C, Lady Jaydee, Dataz, Sister P ambao ndio kidogo walionyesha kudumu kwa muda mrefu katika mziki wa Bongo, lakini hivi sasa zimekuja sauti mpya chipukizi ambazo ndio zimeonekana kuanza kuuteka mziki wa Bongo Flava katika upande wa Wasichana.

Mwandishi wa Makala hii, amefatilia mziki wa Bongo Flava kwasasa katika upande wa Wanawake na kugundua kwamba upande huu kuna sura nyingi mpya tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

LULU DIVA

Wakati anaanza wengi waliona kama vile ni miongoni mwa watu wanaokuja kuzingua katika mziki wa Bongo flava, lakini kadri siku zinavyokwenda ndio anazidi kuwa mcharo.

Awali miezi saba iliyopita aliachia ngoma yake ya ‘Give it to Me’, lakini baada miezi miwili akaja kuachia ngoma nyingine ‘Utamu’, baada ya hapo akasikilizia upepo jinsi ulivyoenda kisha mwezi uliopita ameachia kibao chake cha ‘Mazoea’, ngoma hii imeonyesha kabisa kwamba bado yupo katika game hii licha ya kukaa kimya kwa miezi kadhaa.

Uwezo wake ni mkubwa kwasababu anaweza kuimba mchiriku kama ambavyo amefanya katika ngoma yake mpya ya mazoea, lakini vile vile anaweza kuimba nyimbo za mapenzi kama ilivyo katika ‘Give it to me’.

Kwa staili yake hii atakaa kwa muda mrefu katika game ya bongo kwa sababu wasanii wengi wa kike hata kiume wanashindwa kubadilika kuendana na muda, mashabiki wanahitaji nini.

NANDY

Huyu ndiye mrembo ambaye hivi sasa anatamba vilivyo katika anga za bongo flava, hii ni kutokana na jinsi ambavyo sauti yake inavyokonga nyoyo za wasikilizaji wa mziki wa Bongo.

Anatamba na ngoma yake “Kivuruge” pamoja na “Subalkheri” aliyofanya na Aslay, ngoma zote hizi zote zinasikika vilivyo mtaani mpaka katika kumbi za starehe.

Msanii kama huyu anabidi aongeze spidi ya kutosha kwasababu hata miaka ya nyuma kulikuwa na wadada warembo kama yeye ambao walipanda ghafla, lakini nao walijikuta wameshuka kama vile maji kwenye ardhi na kupotea kabisa katika masikio ya mashabiki wa muziki mzuri.

ROSA LEE

Miongoni mwa wadada ambao wamebaki katika uchanaji, miaka ya nyuma kulikuwa na Sister P,Zay B, akaja Chiku Keto, lakini mwisho wa siku wakapotea kabisa wote.

Ameonekana kuwa na staili ya kipekee katika uchanaji wake hasa akiimba kama vile hataki huku akiweka staili za kiume zaidi huku muonekano wake ukiwa wakiume zaidi.

Rosa hivi sasa anatamba na ngoma ya “Dow” pamoja na “Marathon”, ngoma ambayo amefanya na Billnas, lakini ngoma zake zote zinaonekana kabisa kwamba zimeanza kukita masikioni mwa mashabiki wao.

AMBER LULU

Alikuwa mtu wa kutengeneza kiki sana, hakuna aliyekuwa anaweza kuja kuimba siku moja kutokana na mara kwa mara alikuwa akionekana katika video za wenzake (Video Vixen),

Staili yake ya nywele kama mwanadada mrembo wa Marekani (Amber Rose), ndio sababu kubwa kwake kuitwa Amber Lulu, lakini hivi sasa amekuja kuwa mcharo katika mziki wa Bongo kama ilivyokuwa kwa mwenzake Gigy Money.

Awali alitamba na ngoma zake “Only You” pamoja na “Jiachie” aliyofanya na Country Boy na hivi sasa anatamba na kibao chake kipya “Jini kisirani” ambacho kimekuwa gumzo mtaani kutokana na maneno aliyoyaimba ndani.

VANESSA MDEE

Muonekano wake tu ni biashara tosha. Mlimbwende huyu pia ni mara chache sana kuonekana mara kwa mara katika matukio akiwa na wenzake.

Lakini katika upande wa kazi dada huyu mwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake Jux, amekuwa akifanya vizuri kuanzia katika tungo mpaka video zake.

Kingine ambacho kinaendeleza ubora wake, ana mtandao mkubwa na wasanii wengine wa nje ya nchi hivyo ngoma zake zinakuwa zinaseogea vilivyo kwenda mbele na mara kwa mara amekuwa akichukua tuzo nje hata asipochukua basi anakuwa yupo katika watu wanaopigania kupata tuzo.

MAUA SAMA

Amekosekana katika kipande cha kufungiwa baada ya kuhusika katika ngoma ya Kiba_100, ambayo alishirikishwa na Kundi la Rostam ambao walifungiwa kujihusisha na mziki.

Maua sama sauti yake licha ya kuwa kama inakwaruza fulani, imefanya ngoma kali kama ‘Hata Sielewi’ ya Fa, lakini pia yeye mwenyewe anatamba na kibao chake kipya cha ‘Nakuelewa’, ambacho nacho kinatamba vilivyo hivi sasa.

CHEMICAL

Inawezekana hivi sasa mziki wa Bongo flava kwa upande huu umekuwa sawa, baada ya wadada hawa kugawana vizuri katika upande wa kuimba mpaka kuchana (kurap).

Mdada huyu alikuja kabisa kuchukua ile sehemu ambayo iliachwa na msanii Chiku Keto ambaye alikuwa akipiga mapigo ya kiume siku za nyuma, lakini hivi sasa amepotea kabisa katika ulimwengu huu wa muziki.

Chemical alianza mdogomdogo na ngoma zake za kukaza kama Mary Mary, Struggling, lakini naye akaanza kulegeza uzi mpaka hivi sasa kuanza kuimba nyimbo nyepesi kama Asali aliyofanya na Beka Flavour, kwa kubadilika badilika kwake kunamfanya azidi kuendelea kuwepo katika game hii ya mziki na kuziba baadhi ya mapengo ya awali ambayo yaliachwa na wasanii wengine.