Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapinzani wa Yanga CAF waitaja Simba

CAF Pict

Muktasari:

  • Connor ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Cape Town Spurs ya Afrika Kusini, amesema anataka kufanya maajabu kwa kuishangaza Yanga inayofundishwa na Manqoba Mngqithi, huku akibainisha kwamba hawatarudia makosa kama ilivyokuwa walipokutana na Simba msimu uliopita.

KOCHA wa Gaborone United, Sean Connor, amesema licha ya kufahamu ugumu wa kuikabili Yanga katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kuna mkakati wanauweka kuhakikisha wanavuka salama.

Connor ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Cape Town Spurs ya Afrika Kusini, amesema anataka kufanya maajabu kwa kuishangaza Yanga inayofundishwa na Manqoba Mngqithi, huku akibainisha kwamba hawatarudia makosa kama ilivyokuwa walipokutana na Simba msimu uliopita.

Yanga inaanzia ugenini safari yake ya kimataifa msimu ujao 2026-2027 kwa kukutana na Gaborone United ya Botswana, huku kila upande ukihitaji kufanya vizuri kuvuka hatua hiyo.

Akizungumzia kukutana na Yanga, Connor amesema: “Yanga ni miongoni mwa timu zenye historia kubwa zaidi nchini Tanzania. Walifika fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF miaka michache iliyopita.

CA 01

“Katika misimu mitatu au minne iliyopita wamekuwa wakifika hatua ya makundi, na hivi karibuni walifika pia hatua ya robo fainali. Kwa hiyo, hakuna shaka kwamba hii ni kazi kubwa kwetu. Lakini kama unataka kucheza katika kiwango hiki, lazima ukutane na kucheza dhidi ya timu bora.”

Kocha huyo raia wa Ireland Kaskazini, aliendelea kwa kusema:

“Nilikuwa nikisubiri kwa hamu kujua tutapangiwa nani katika mashindano ya CAF, na inaonekana safari hii tunapaswa kucheza dhidi ya timu ya Tanzania, kama ilivyokuwa msimu uliopita.

“Msimu uliopita tulicheza dhidi ya Simba. Wachezaji walikuwa na mtazamo chanya na pengine tulikuwa na bahati mbaya ya kupoteza mchezo huo.

“Kwa hiyo, mchezo huu unaokuja ni mechi ambayo wao ndio wanaopigiwa upatu kuwa washindi, lakini tukijituma, tukatumia vizuri nafasi zetu na tukapata bahati kidogo, tunaweza kusonga mbele hadi hatua ya makundi.”

Mshindi wa mechi hii, atakwenda kucheza dhidi ya mshindi kati ya CFFA ya Madagascar au Lijabatho ya Lesotho kuwania kufuzu makundi.

CA 02

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Gaborone United kucheza dhidi ya timu ya Tanzania baada ya msimu uliopita kuondoshwa na Simba kwa jumla ya mabao 2-1. Mechi ya kwanza nchini Botswana, Simba ilishinda 1-0, ziliporudiana Dar es Salaam, matokeo yakawa sare ya 1-1.

Yanga msimu wa 2026-2027 ina malengo ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya CAF baada ya 2025-2026 kuishia makundi ikimaliza nafasi ya tatu kundi B ikikusanya pointi nane, ikishinda mechi mbili sawa na sare na ilizopoteza baada ya kushuka dimbani mara sita.

Katika kampeni yake ya kufuzu makundi msimu huo, Yanga iliitoa Wiliete ya Angola kwa jumla ya mabao 5-0 kwenye hatua ya awali, kisha hatua ya pili ikaiondosha Silver Strikers ya Malawi kwa mabao 2-1.

Gaborone United msimu uliopita iliishia hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiondoshwa na Simba kwa jumla ya mabao 2-1.