Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita tatu Ligi Kuu Bara

VITA Pict

Muktasari:

  • Mechi ya kwanza itakuwa Arusha kuanzia saa 10:00 jioni ambapo TRA United inarudi nyumbani ikiikaribisha Dodoma Jiji iliyoanza msimu vibaya, hapa zinakutana timu mbili ambazo hazijapata ushindi wowote kwenye mechi tatu za kwanza.

LIGI Kuu Bara inaendelea leo Jumamosi ambapo timu sita zitakuwa viwanjani kuamua vita ya pointi na kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo.

Mechi ya kwanza itakuwa Arusha kuanzia saa 10:00 jioni ambapo TRA United inarudi nyumbani ikiikaribisha Dodoma Jiji iliyoanza msimu vibaya, hapa zinakutana timu mbili ambazo hazijapata ushindi wowote kwenye mechi tatu za kwanza.

TRA ikiwa inatoka kwenye mechi tatu za ugenini ikipoteza moja dhidi ya Azam (2-1), kisha sare mbili zinazofanana ilipokutana na JKT Tanzania na Coastal Union ikifungana nazo kwa bao 1-1, inarudi nyumbani kutafuta ushindi wake wa kwanza ikiwa na pointi zake mbili.

Kitu pekee bora ambacho TRA inaweza kuanzia nacho ni kwamba kikosi hicho kimefanikiwa kufunga bao katika kila mchezo, ambapo itatakiwa kuimarisha safu yake ya ulinzi ambayo nayo imeruhusu mabao manne kwenye mechi tatu.

Kocha wa TRA, Etienne Ndayiragije akizungumzia mchezo huo, amesema wanarudi nyumbani wakiwa na akili moja tu ya kutafuta ushindi wa kwanza, akiringia ubora wa wachezaji wake.

“Wachezaji walipambana sana kwenye mechi hizi tatu za kwanza, kuna changamoto tunatakiwa kuzifanyia kazi lakini kitu muhimu hapa ni kwamba tumerudi nyumbani tumefanikiwa kupata pointi mbili pekee tukiangusha sita, tunataka kuona ushindi wetu wa kwanza ukianzia nyumbani,”  amesema Ndayiragije.

VIT 01

Dodoma yenyewe haijashinda mechi yoyote, ikianza msimu kwa sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Pamba Jiji, kisha kupoteza mbele ya Mbeya City na mechi ya nyumbani ilipokutana na Polisi Tanzania. Kwenye mechi hizo tatu, Dodoma imeruhusu mabao manne, ikicheza mechi mbili bila kufunga bao lolote dhidi ya Mbeya City na Polisi Tanzania, ikifunga bao moja pekee.

Kocha wa timu hiyo Mnyarwanda, Vicent Mashami akizungumzia mchezo huo amekiri kuanza vibaya kwa kikosi chake akisema wamejipanga kutafuta matokeo mazuri zaidi ya ushindi dhidi ya TRA huku wakijua ubora wa wenyeji wao.

“Ni ukweli uliowazi kwamba hatujaanza msimu vizuri, tumekuwa na matokeo ambayo hayavutii, hatustahili hili, tunahitaji kubadilika haraka, nimewaambia wachezaji wangu namna ya kutoka hapa, tuna lengo moja tu kesho (leo) kutafuta ushindi ingawa tunafahamu tunakwenda kukutana na timu nzuri,” amesema Mashami.


VIT 02

SINGIDA VS POLISI TANZANIA  

Mchezo mwingine utakuwa pale Singida kuanzia saa 12:30 jioni, ambapo wenyeji Singida Black Stars inayotoka kwenye maumivu itawakaribisha Polisi Tanzania iliyorejea ligi kuu kwa kishindo kikubwa.

Singida ilianza msimu vizuri, ikishinda nyumbani 3-0 dhidi ya Fountain Gate, kisha kulazimishwa sare ugenini ya bao 1-1 ikikutana na Kagera Sugar, ikapata kipigo cha kwanza cha mabao 2-1 nyumbani kutoka kwa Simba.

Singida katika ufungaji haina mashaka sana, ikifunga mabao matano kwenye mechi tatu huku eneo la ulinzi likiruhusu mabao matatu, ikienda kutafuta ushindi wa pili msimu huu.

Kocha wa Singida, Mkongomani Pappy Kimoto amesema wanajua walikosea wapi dhidi ya Simba, wakiheshimu kuwa Wekundu hao walikuwa na ubora, lakini wanautaka ushindi wa pili nyumbani mbele ya Polisi. “Timu tunakwenda kukutana nayo ni nzuri imekuwa na matokeo mazuri, lakini tunajua kwamba hatukuwa na matokeo mazuri kwenye mechi dhidi ya Simba, ilikuwa mechi kubwa, tunataka kubadilisha matokeo haya kwa kurudi kwenye ushindi,”  amesema Kimoto, kocha wa zamani wa Union Maniema ya DR Congo.

Polisi Tanzania imerejea kwa kishindo ikiilazimisha sare ya bao 1-1 Azam, kisha ikaichapa JKT Tanzania 2-0, ugenini ikaipiga Dodoma Jij. Ikicheza mechi mbili za mwisho bila wavu wake kuguswa, ikikusanya pointi saba.

Kocha wa timu hiyo, Mbwana Makata aliowarudisha ligi kuu, akizungumzia mchezo huo amesema: “Haitakuwa mechi rahisi lakini najivunia morali ya wachezaji wangu, tutakwenda kutumia ubora wetu kushindana na timu yenye wachezaji bora.”


VIT 03

JKT TANZANIA VS NAMUNGO

Mchezo wa mwisho utakuwa pale Meja Jenerali Isamuhyo ambapo JKT Tanzania iliyoanza msimu kichovu itawakaribisha Namungo kuanzia saa 3:00 usiku.

JKT Tanzania ilianza msimu kwa sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya TRA Utd, kisha ikapoteza mbili za ugenini (2-0) dhidi ya Polisi Tanzania, kisha kipigo kikali kutoka kwa bingwa mtetezi Yanga (4-0).