Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker amwaga sifa Msimbazi, asaka jambo jipya

BARKER Pict


SIMBA imeshinda mechi zake nne za kwanza katika Ligi Kuu Bara msimu huu, ikiwa na asilimia mia ya ushindi wake, hata hivyo mashabiki wa timu hiyo bado hawaridhiki sana kwa namna ya uchezaji wanaouona, hali hiyo imemfanya kocha Steve Barker kupanga kukomaa na jambo moja.


Timu hiyo imeshinda mechi nne ikizipiga Kagera Sugar (2-0), Pamba Jiji (2-1), Singida Black Stars (2-1), kisha kuichapa Coastal Union (1-0) kwenye mechi ya kwanza nyumbani msimu huu.


Akizungumza na Mwanaspoti, Barker amesema, licha ya kuanza kibabe ligi, lakini bado anataka kuona ubora wa kutumia nafasi ambazo wanatengeneza kwenye mechi.

ISA 01

Barker amesema kikosi chake kina ubora mkubwa wa kutengeneza nafasi, lakini kitu ambacho watako maa nacho sasa ni kuhakikisha wanaongeza ufanisi wa kuzitumia kwa kutengeneza mabao ya kutosha.

“Tumekuwa bora kwenye kutengeneza nafasi lakini nafahamu kuna kiu ya kuona tunafunga zaidi, tunahitaji kuliongezea umakini hilo, unapotumia nafasi nyingi unaifanya mechi kuwa rahisi, unaposhindwa kutumia nafasi unawapa nguvu wapinzani,”  amesema Barker.

ISA 02

Ni na furaha kwamba jambo la msingi ni kutenegeza ushindi hili lipo sawa lakini bado tuna nafasi ya kuimarisha ushindi wetu, hili tutaliboresha taratibu kuanzia eneo la mazoezi.

Barker amesema jambo ambalo limemvutia kwenye kikosi chake ni namna wachezaji kutoka idara zote wanavyoonyesha ubora wa kupigania matokeo ambapo kila eneo limeshatengeneza wafungaji.

“Tunashinda, sifa kubwa nitazipeleka kwa wachezaji wote. Mpaka sasa unaona namna tunavyonyesha kucheza kama timu kwa mabeki wanafunga, eneo la kiungo nalo likitoa wafungaji na hata kule mbele nako tukionyesha kitu ingawa bado tunataka kikubwa zaidi.

ISA 01 (1)

“Msimu uliopita Simba ndio timu iliyozalisha mechi nyingi ngumu na msimu huu hilo limeendelea kuonekana, kila mechi inakuwa na uzito mkubwa na bado tumeweza kuonyesha na kupata kile ambacho tunataka,” amesema Barker.

Katika mechi nne ambazo Simba imecheza, mabao yake yamefungwa na mabeki Ismael Toure aliyefunga mara mbili, Rushine De Reuck, viungo wakiwa Clataous Chama akifunga mara mbili, Anicet Oura na Elie Mpanzu.