Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulinzi waimarishwa uwanja wa Uhuru Simba Day

Muktasari:

  • Uwepo wa walinzi wenye silaha, umeonekana zaidi katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, huku wakifuatilia utaratibu hasa wa kuingia na kutoka katika uwanja huo. Jambo hilo limeongeza hali ya utulivu kwa mashabiki wanaoingia uwanjani.

ULINZI umeimarishwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, linapofanyika tamasha la Simba Day, huku shughuli mbalimbali zikiendelea na watu wakizidi kuwasili eneo hilo. Walinzi wameonekana katika maeneo tofauti ya uwanja wakihakikisha hali inabaki kuwa shwari.

Uwepo wa walinzi wenye silaha, umeonekana zaidi katika maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu, huku wakifuatilia utaratibu hasa wa kuingia na kutoka katika uwanja huo. Jambo hilo limeongeza hali ya utulivu kwa mashabiki wanaoingia uwanjani.

Mbali na walinzi, maeneo muhimu ya uwanja kama geti la kuingilia mashabiki yanaendelea kuangaliwa kwa karibu ili kuzuia vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa watu. Huku mashabiki wakionekana kufuata maelekezo yanayotolewa na wahusika wa usalama.

Kwa kuwa idadi ya watu imekuwa ikiongezeka, uangalizi umeendelea kuwa muhimu kuhakikisha hakuna msongamano unaoweza kusababisha usumbufu au changamoto za kiusalama.

Hali ya uwanja imeendelea kuwa tulivu, huku vikosi vya ulinzi vikiendelea na majukumu yao kuhakikisha shughuli zinaendelea bila vurugu wala usumbufu.