Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hali ilivyo Uwanja wa Uhuru

Muktasari:

  • Bado mashabiki wanaendelea kuingia uwanjani, huku makundi mbalimbali ya wapenzi wa Simba yakiendelea kuwasili yakiwa yamevalia jezi nyekundu na nyeupe. Pia rangi ya bluu ipo.

SAA 9:30 alasiri, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam unaendelea kuchangamka huku mashabiki wa Simba wakizidi kumiminika kwa wingi kuingia uwanjani kushuhudia kilele cha Simba Day 2026, ambapo mwaka huu tamasha hilo linafanyika sambamba na maadhimisho ya miaka 90 ya klabu hiyo.

Bado mashabiki wanaendelea kuingia uwanjani, huku makundi mbalimbali ya wapenzi wa Simba yakiendelea kuwasili yakiwa yamevalia jezi nyekundu na nyeupe. Pia rangi ya bluu ipo.

Hali hiyo imefanya mazingira ya nje na ndani ya Uwanja wa Uhuru kuendelea kuwa na shamrashamra, huku mashabiki wakionekana kuwa na hamu ya kushuhudia matukio mbalimbali yaliyoandaliwa na klabu yao katika siku hiyo maalumu.

Simba Day ya mwaka huu imekuwa na mvuto wa aina yake kutokana na Simba kutimiza miaka 90 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1936, jambo lililoongeza hamasa kwa mashabiki walioamua kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maadhimisho hayo.

Uwanja wa Uhuru umechaguliwa kuwa mwenyeji wa tukio hilo kutokana na Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa katika kipindi cha ukarabati kuelekea AFCON 2027.