Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Day mtoko uzi mpya

Muktasari:

  • Mashabiki wengi wa Simba waliofika hapa wametinga jezi nyingi mpya ambazo zilizinduliwa wiki chache zilizopita, uzinduzi uliofanyika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.

HAPA Uwanja wa Uhuru, jezi nyingi ambazo zimevaliwa na mashabiki wengi ni zile mpya za msimu ujao 2026-2027, huku zile za misimu iliyopita zikiwa chache.

Mashabiki wengi wa Simba waliofika hapa wametinga jezi nyingi mpya ambazo zilizinduliwa wiki chache zilizopita, uzinduzi uliofanyika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Jezi nyingi mpya ambazo zinatamba hapa uwanjani ni zile nyekundu, zinafuatia nyeupe huku za bluu zikiwa kwa uchache.

Jezi za msimu uliopita nyingi ambazo zimevaliwa hapa uwanjani ni zile nyekundu ambazo nazo bado zinauzwa hapa kwenye mabanda tofauti ya wafanyabiashara.

Mashabiki wengi wanadai jezi nyekundu za msimu ujao zimetulia zaidi zikiwa na rangi halisi ya kwanza ya klabu hiyo huku wanawake wakizipenda zaidi nyeupe wakisema zinavutia kwa rangi yake ukichanganyika na pinki.

Waliovaa jezi za bluu wanazisifia wakidai zinapendeza kwa kuwa hazichagui sana kwamba yeyote au ukivaa na nguo yoyote utapendeza.