Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ulimwengu aipeleka Mazembe makundi

USHINDI wa mabao 2-1 walioupata TP Mazembe umetosha kusonga hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mabao hayo yamefungwa na Mshambuliaji wa Kitanzania, Thomas Ulimwengu.

Ulimwengu amefikisha mabao matatu kwenye michuano hayo ambapo mechi hiyo ya marudiano na Bouenguidi ya Gabon imechezwa Uwanja wa TP Mazembe, DR Congo.

Ulimwengu ndiye alianza kutikisa nyavu za wapinzani wake dakika ya 14 kabla ya Mwape kongeza bao la pili dakika ya dakika ya 45  huku wapinzani wao  wakifunga bao moja kipindi cha pili dakika ya 78.

Mazembe wamesonga mbele ekwa jumla ya mabao 4-2 kwani mechi ya kwanza pia waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mabao ambayo yote yalifungwa na Ulimwengu.