Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaigeuza ngazi Simba, ikibeba Ngao tena

Muktasari:

  • Bao la kiungo mshambuliaji, Albert Kangwanda dakika ya 31, limetosha kuipa Yanga ushindi huo akifunga kwa kichwa akitumia krosi ya beki wa kushoto, Chadrack Boka.

YANGA imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba ikijihakikishia ubingwa wa Ngao ya Jamii kwa mara ya tatu mfululizo.

Bao la kiungo mshambuliaji, Albert Kangwanda dakika ya 31, limetosha kuipa Yanga ushindi huo akifunga kwa kichwa akitumia krosi ya beki wa kushoto, Chadrack Boka.

Simba kabla ya kuruhusu bao hilo, ilifanikiwa kucheza vizuri kwa kuipa presha Yanga kwa mashambulizi makali dakika 15 za kwanza, lakini hayakuwa na madhara kwenye ukuta wa watani wao.

Simba baada ya bao hilo, ikairuhusu Yanga kutawala mchezo huo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ikibanwa maeneo mengi ikishindwa kutengeneza mashambulizi tena.

Dakika ya 37, mshambuliaji wa Yanga, Peter Shalulile alipoteza nafasi ya wazi kuipa timu hiyo bao la pili wakati lilipotengenezwa shambulizi la haraka, shuti lake likatoka nje kidogo.

Mapumziko, Yanga ikatoka na uongozi wa bao 1-0 huku ikitawala vizuri mchezo wakati Simba ikishindwa hata kuwa na shuti moja lililolenga lango.

Kipindi cha pili timu hizo zikaendelea kushambuliana ambapo licha ya Simba kurudi na mabadiliko ikimtoa mshambuliaji Ibrahim Doumbia akiiingia Elie Mpanzu, lakini bado hayakuweza kusaidia.

Simba ikapoteza nafasi nzuri kwenye mchezo huo dakika ya 89 kupitia kiungo mshambuliaji Bakari Msimu aliyeingia kipindi cha pili, shambulizi lake likapanguliwa na kipa Djigui Diarra kisha kuwahi kuudaka tena.

Mpaka mwisho wa mchezo, Yanga ikafanikiwa kutoka na ushindi huo, ikitetea taji hilo ikilichukua mara ya pili mfululizo mbele ya Simba ikifanya hivyo 2025 na 2026 na zote ikishinda kwa bao 1-0.

Kabla ya hapo, 2024, Yanga iliifunga Azam mabao 4-1 na kubeba Ngao ya Jamii. Sasa Yanga imechukua Ngao ya Jamii mara kumi tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2001, ikiwa ndiyo timu kinara.