Twende zetu Ivory Coast Ki-VIP kumenoga
Wakati washindi sita wa kampeni ya Twende Zetu Ivory Coast Ki-VIP wakitarajiwa kutangazwa Januari 2, kampeni hiyo imeendelea kutoa zawadi mbalimbali za siku na za wiki kote nchini.
Iko hivi, mashabiki wa soka nchi wamepewa fursa ya kuishuhudia kibabe fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani, wakiishuhudia mubashara timu ya Tanzania (Taifa Stars) ikipeperusha bendera kwenye fainali hizo nchini Ivory Coast kwa gharama za Betika.
Fainali hiyo itaanza Januari 13 – Februari 11 nchini Ivory Coast na washindi sita wanaobashiri na Betika kupitia Tigopesa watakwenda kuishuhudia Afcon hiyo bure kule Ivory Coast, Betika ikigharamia kila kitu.
Kabla ya droo hiyo kubwa ya Januari 2, Betika na Tigopesa wamekuwa wakitoa zawadi mbalimbali kwa washindi wanaoendelea kubashiri.
"Leo tunakabidhi TV (Luninga) ya nchi 70 kwa mmoja wa washindi wetu wa wiki, Emmanuel Anderson," amesema Martin Mavula, Meneja wa Tigo Dodoma.
Awali, ofisa habari wa Betika, Rugambwa Juvelinaus alisema kampeni hiyi inatoa washindi wawili wa Luninga nchi 70 kila wiki.
"Hawa wanapata na dikoda yenye kifurushi, vilevile kuna mamilioni ya pesa kwa washindi wa kila siku.
"Unapoendelea kubashiri nasi kupitia akaunti ya Tigopesa ndipo unajiweka kwenye nafasi kubwa ya kushinda zawadi mbalimbali na kuingia kwenye droo ya Twende zetu Ivory Coast Ki-VIP," amesema.
Mbali na ushindi kwa wateja wa Betika, Rugambwa amesema:"Timu yetu ya taifa inahitaji sapoti ya Watanzania, Betika kwa kutambua hilo tukaona tutoe fursa hii, lakini ni kwa wale tu wachezaji wetu wanaotumia Tigopesa,".
Stars itashiriki Afcon kwa mara ya tatu msimu ujao, baada ya ile ya 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri.
Msimu huu Stars ilifuzu baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi F na kumaliza kundi hilo ikiwa na pointi nane, nyuma ya vinara, Algeria wenye pointi 16 na wote kufuzu wakizipiku Uganda iliyomaliza na pointi saba na Níger pointi mbili.
Balozi wa Betika Dodoma, Sara Sarakikya amesema ni rahisi kupata nafasi ya kwenda Ivory Coast kushuhudia mubashara Afcon.
"Unachotakiwa ni kuweka pesa kwenye tigopesa yako na kubeti na Betika," amesema na kuongeza.
"Pia zawadi nyingine za kila siku na kila wiki za pesa taslimu na luninga, inaendelea hadi Januari 2 itakapofanyika droo ya washindi sita wa kwenda Ivory Coast kwenye Afcon.