Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taswira ya Dabi inaanzia hapa

DABI Pict

Muktasari:

  • Matamasha hayo yanafanyika siku chache kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaozikutanisha timu hizo ambao utachezwa Jumatano ijayo, Agosti 12, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Zanzibar.

WIKIENDI hii kuna matamasha yanayoandaliwa na klabu kongwe hapa nchini, Simba na Yanga. Leo Jumamosi ni Simba Day, kesho Jumapili ni Yanga Day.

Matamasha hayo yanafanyika siku chache kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaozikutanisha timu hizo ambao utachezwa Jumatano ijayo, Agosti 12, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Zanzibar.

Mwanaspoti limefanya mahojiano kwa nyakati tofauti na mastaa wa zamani wa klabu hizo, ambapo wamesema watapata nafasi ya kuzitazama Simba na Yanga kupitia matamasha yao hayo kabla ya kushuhudia Dabi ya Kariakoo.

DAB 01

Staa wa zamani wa Simba, Zamoyoni Mogella, amesema klabu hizo kusajili ni jambo moja, wachezaji kucheza kwa kiwango wanachotarajiwa ni jambo lingine. “Ni kweli tumeziona Simba na Yanga zimesajili, ingawa kwa udogo tuzione katika mechi za matamasha yao, ila kwa sasa itakuwa ngumu kuona mechi ya Ngao ya Jamii itakuwaje kwa pande zote mbili,” amesema.

Mtazamo wa Mogella haukupishana na wa staa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila ambapo amesema: “Yanga haijacheza mechi zaidi ya kufanya mazoezi na Simba nimeona katika michuano ya Cecafa Kagame Cup 2026, asilimia kubwa wamecheza wachezaji wao wa zamani, hivyo hizo timu zikicheza mechi za matamasha yao ndipo tutakapopata picha ya dabi itakuwa ya aina gani.”

DAB 02

Mwingine aliyechangia hilo ni beki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Oscar Joshua, aliyesema: “Angalau timu hizo zicheze mechi za matamasha yao, ingawa pia haziwezi kutoa taswira kamili lakini mwanga utaonekana dabi itakuwa ya aina gani.”

DAB 03

Wakati mtazamo wa mshambuliaji wa Simba na Taifa Stars, Emmanuel Gabriel ulikuwa ni: “Mabadiliko ya wachezaji yaliyofanywa na hizo klabu, yataleta vionjo vipya vya mechi angalau tuone zitakavyocheza mechi za matamasha ndipo tutakapojua ushindani wa bato utakuwa eneo lipi, baada ya hayo matamasha angalau tutakuwa na mwanga wa kuzungumzia Ngao ya Jamii.”

Mechi ya Ngao ya Jamii iliyopigwa Septemba 16, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga ilishinda bao 1-0, mfungaji akiwa Pacome Zouzoua dakika ya 54.