Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa Msuva arejea zake Morocco

BAADA ya muda wake wa mapumziko mafupi kumalizika nchini, mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva amerejea zake Morocco kuendelea na majukumu yake ya kuitumikia, Wydad Casablanca.

Msuva alipewa mapumziko hayo mafupi ambayo yalimalizika, Jumamosi baada ya majukumu mazito ya kitaifa aliyokuwa nayo ya kuipigania Taifa Stars kucheza michezo miwili ya kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika.

Hata hivyo juhudi za Msuva na wachezaji wenzake wa Taifa Stars ziligonga mwamba baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 wakiwa ugenini dhidi ya wenyeji wao, Guinea ya Ikweta hivyo ushindi dhidi ya Libya ulishindwa kuwabeba.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, ameondoka nchini kibabe huku akitamba kwamba pindi atakaporejea anaweza kurudi na medali ya kutwaa Ligi ya Mabingwa Afrika au Ligi Kuu Morocco maarufu kama Batola Pro.

“Naenda kuendelea na mapambano ambayo yapo mbele yetu, Wydad ni klabu ya mataji hivyo kila msimu wamekuwa wakipambania mataji, roho hiyo imeniingia na kujikuta nikiwaza mataji kila wakati, naamini hilo nitalitimiza,” alisema.

Msuva ambaye chama lake limetinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, anatarajiwa kuwa sehemu ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Morocco ambao utachezwa keshokutwa, Jumatano dhidi ya Rapide Oued Zem.

Wydad Casablanca wanaongoza msimamo wa Batola Pro wakiwa na pointi 22 kileleni huku wakifuatiwa na mahasimu wao, Raja Casablanca wenye pointi 19.