Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichoibeba Tanzania ubingwa FIBA Zone V

Muktasari:

  • Tanzania ilitwaa ubingwa huo katika hatua ya kwanza ya mashindano ya FIBA Africa Zone V, na ushindi huo umeiwezesha kufuzu hatua inayofuata ya mashindano hayo itakayofanyika nchini Rwanda mwakani.

BAADA ya timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 16 kutwaa ubingwa wa Kanda ya Tano ya Afrika, baadhi ya wachezaji wamesema nidhamu na usikivu wa maelekezo ya makocha yalikuwa miongoni mwa mambo yaliyowasaidia kufanikisha ushindi huo.

Tanzania ilitwaa ubingwa huo katika hatua ya kwanza ya mashindano ya FIBA Africa Zone V, na ushindi huo umeiwezesha kufuzu hatua inayofuata ya mashindano hayo itakayofanyika nchini Rwanda mwakani.

Tanzania ilifuzu baada ya kuifunga Kenya katika michezo miwili iliyofanyika mjini Mombasa, Kenya, kwa pointi 62-52 na 70-60.

Akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) katika Hoteli ya Serena, mmoja wa wachezaji hao, Sarfu Hassan, alisema walijituma kwa muda wote wa mchezo na kufuata maelekezo ya makocha wao. “Hata kama tumechoka, tulikuwa hatuonyeshi kama tumechoka. Tulikuwa tunapambana huku tukisikiliza maelekezo ya makocha wetu,”  alisema Hassan.

Naye Sheth Cothema alisema kila mchezaji alijitoa kwa ajili ya kuisaidia Tanzania kutwaa ubingwa huo. “Tulicheza huku nyuma yetu tukijua Watanzania wako pamoja nasi na wanatupa moyo,”€  alisema Cothema.

Baada ya ushindi huo, Rais wa TBF, Hasheem Thabeet, aliwapongeza wachezaji hao kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kulileta kombe nchini, huku akiwataka makocha kuandaa ratiba nzuri ya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya hatua inayofuata.

Naye kiongozi wa timu ya Dar City, Mussa Mzenji, aliwataka vijana hao kuendelea kujituma na kutokata tamaa, akiwahimiza kutumia fursa zilizopo katika michezo, ikiwemo uwezekano wa kupata nafasi za masomo nje ya nchi.