Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sowah afunguka dili la Simba, akituma salamu mapema

SOWAH Pict


MABOSI wa Simba wameendelea kukisuka kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao wa 2025-2026 kwa kushusha mashine za maana kimyakimya, huku ikielezwa imeshamalizana na straika aliyekuwa Singida Black Stars, Jonathan Sowah.


Mwanaspoti lililoripoti mapema juzi kuwa, straika huyo anajiandaa kusaini mktaba wa miaka miwili kukipiga Msimbazi, imepata nafasi ya kuzungumza na Sowah ambaye ni raia wa Ghana aliyefunguka kila kitu kilichomfanya atue Simba na kutuma salamu mapema kwa mabeki wa timu pinzani.


Sowah kwa kinywa chake amethitisha kwamba msimu ujao anahamishia shughuli ya kutikisa nyavu akiwa na jezi za Simba, lakini akaweka hesabu zake huku akiwatumia ujumbe maalum mashabiki wa wekundu hao.

Akizungumza na Mwanaspoti moja kwa moja kutoka Ghana Sowah, alisema wakati akimalizia mapumziko yake ameanza kujiandaa kujipanga na maisha mapya ndani ya klabu hiyo kubwa aliyojiunga nayo kwa mkataba wa miaka miwili.

Sowah, alisema anapoelekea Simba, anakwenda kuendelea kuthibitisha ubora wake kwa kufunga mabao zaidi kama ambavyo alifanya wakati akiwa na Singida Black Stars.

Sowah akiwa Singida akiichezea nusu msimu tu kwenye mzunguko wa pili, alitumia mechi 13 kufunga mabao 13, akikosa kufunga kwenye mechi mbili pekee, ikiwemo moja ya wekundu hao kwenye ligi.

"Nimeshajulishwa na viongozi wa klabu kwamba, nakwenda Simba, nina furaha ya kwenda kujiunga na timu hiyo kubwa Afrika, kwasasa najipanga kuanza maisha mapya namalizia mapumziko nakuja hivi karibuni,"alisema Sowah.

"Mimi ni mchezaji ninayejua majukumu yangu, nadhani mliona ndani ya nusu msimu tu nilifanya kitu gani nikiwa na Singida Black Stars, kwangu kwenda kujiunga na Simba ni kwenda kuendeleza ubora wangu kwa kufunga zaidi.

Aidha Sowah akizungumzia mivutano na mashabiki wa Simba alisema kila mmoja alikuwa anatimiza wajibu wake kwenye hizo mechi na kwamba hana tatizo na mashabiki hao wajipange kufurahia namna atakavyoipigania timu hiyo.

"Nakumbuka ile hali(anacheka), ninachoweza kusema mimi sina matatizo ya nidhamu ndio maana unaona klabu nyingi zinanihitaji, wakati ule ilikuwa natimiza wajibu wangu kuipigania timu yangu na mashabiki nao wakiipigania timu yao.

"Wakati huu nakwenda kuipigania jezi ya Simba kwa nidhamu zote, nitawafanyia kazi ili wafurahi, unajua mimi ni mchezaji ninayependa kufanya vizuri wakati wote ili wale walionyuma yetu wafurahie kazi yangu.

"Nadhani tangu nimekuja hapo Tanzania hukuwahi kusikia Singida wananilalamikia kwamba sina nidhamu, kila kitu kilikuwa sawa ndani ya timu na nawashukuru sana."