Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Toba mikononi mwa Mbeya City

TOBA Pict

Muktasari:

  • Kipa huyo aliyemaliza na clean sheets nne za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, alikuwa katika mazungumzo na timu za Namungo FC, JKT Tanzania na Kagera Sugar, ingawa Mbeya City tayari imefikia katika hatua nzuri ili kuipata saini yake.

UONGOZI wa Mbeya City, uko katika hatua nzuri wa kuipata saini ya aliyekuwa kipa wa Mtibwa Sugar, Toba Kutisha baada ya pande zote mbili kufanya kikao na kukubaliana kila kitu, huku kilichobakia ni nyota huyo kuingiziwa fedha tu ili asaini.

Kipa huyo aliyemaliza na clean sheets nne za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, alikuwa katika mazungumzo na timu za Namungo FC, JKT Tanzania na Kagera Sugar, ingawa Mbeya City tayari imefikia katika hatua nzuri ili kuipata saini yake.

Hata hivyo, JKT Tanzania ilijitoa rasmi kuiwania saini ya nyota huyo baada ya kukamilisha usajili wa kipa, Constantine Malimi aliyecheza naye Mtibwa Sugar, ambaye kwa msimu wa 2025-2026 katika Ligi Kuu Bara alimaliza na clean sheets nne.

TOB 02

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Mbeya City, Gwamaka Mwankota amesema taratibu zote za usajili zinaendelea kwa ajili ya kuboresha kikosi hicho ambapo watakapofikia makubaliano na mchezaji yeyote wanayemuhitaji watatangaza rasmi.

"Hadi sasa mchezaji pekee tuliyemtambulisha ni Ismail Aziz Kader lakini taratibu zingine bado zinaendelea kutokana na ripoti ya benchi la ufundi, tutakapokamilisha tutatangaza na mashabiki zetu wataona wachezaji wapya," amesema Gwamaka.

Sababu inayomfanya Toba kuondoka Mtibwa Sugar ni kutokana na kushuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara hadi Championship msimu wa 2025-2026, ilipomaliza nafasi ya 15 na pointi 27, ikiungana na KMC na Tanzania Prisons iliyoshuka kupitia Play-Off.