Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SMZ na mkakati wa usalama AFCON 2027

AFCON Pict

Muktasari:

  • Kwa Tanzania, mechi zinatarajiwa kuchezwa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Arusha (Uwanja wa Samia Suluhu Hassan) na Zanzibar (Uwanja wa New Amaan Complex na Fumba vilivyopo Unguja).

VIKOSI vya ulinzi na usalama vimetakiwa kuanza ujuzi maalumu utakaotumika katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kwa lengo la kudumisha usalama kipindi chote cha mashindano hayo.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Issa Mahfoudh Haji, wakati akifungua mafunzo ya Maofisa wa Ulinzi yaliyofanyika Tunguu Zanzibar.

​Issa amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo maafisa hao kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuongeza uelewa wa kuisaidia maandalizi ya michezo hiyo.

​"Ulinzi unatakiwa katika maeneo yote yatakayotumika ikiwemo majengo ya michezo, maeneo ya mafunzo, maeneo ya kufikia wageni pamoja na maeneo ya wazi," amesema.

​Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Michezo Zanzibar, Said Mkwawa amesema Zanzibar iko tayari kwa mashindano hayo baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu inayotakiwa na Baraza la Michezo Afrika (CAF).

​Said amesema, maandalizi ya michezo hiyo si jambo dogo bali linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka sekta binafsi na SMZ ili kuhakikisha Tanzania kwa ujumla inapata matokeo mazuri.

​Mafunzo hayo yanahusisha sekta ya ulinzi na usalama kutoka Sekta ya Michezo Zanzibar (ZFF), Ramadhan Abdalla Bakari, akisema yatasaidia kuwajengea uwezo wa kutosha wananchi ili kuwa na usalama wa kutosha wakati wote wa mashindano.

​Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Mjini Magharibi limeanza operesheni maalumu ya kusafisha barabara kuu, maeneo ya biashara na mitaa ili kuhakikisha Usalama na Amani vinaimarika kuelekea mashindano hayo.

Fainali za AFCON 2027 zinatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 19, 2027 hadi Julai 17, 2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.

Kwa Tanzania, mechi zinatarajiwa kuchezwa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Arusha (Uwanja wa Samia Suluhu Hassan) na Zanzibar (Uwanja wa New Amaan Complex na Fumba vilivyopo Unguja).