Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ofisa uhamiaji Ghana kuamua Simba v Might Wonderes CAFCL

Muktasari:

  • Bulu atasaidiwa na waamuzi wenzake raia wa Ghana, Seth Abletor na Richard Kweku Nartey, ambao watakuwa waamuzi wasaidizi, huku Grema Mohammed wa Nigeria akiwa mwamuzi wa nne.

Mwamuzi, Charles Bulu kutoka Ghana ameteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuchezesha mechi ya raundi ya kwanza ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayozikutanisha Simba dhidi ya Mighty Wanderers.

Bulu ambaye pia ni Ofisa Uhamiaji wa Ghana alianza safari yake ya uamuzi wa soka zaidi ya miaka 10 iliyopita, kabla ya kupanda hatua kwa hatua hadi kufikia ngazi ya kimataifa.

Uwezo wake katika ligi ya ndani ulimsaidia kutambuliwa zaidi, hatimaye akafikia hatua ya kuwa mwamuzi wa kimataifa wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) mwaka 2019.

Tangu hapo, Bulu amekuwa akipewa nafasi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa, ikiwamo yale yanayosimamiwa na CAF.

Kwa mujibu wa rekodi za mashindano mbalimbali, Bulu ameshachezesha zaidi ya michezo 20 ya mashindano ya CAF, ikiwamo mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) pamoja na Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Kabla ya uteuzi wake wa mchezo wa Simba dhidi ya Mighty Wanderers, moja ya mechi zake za karibuni za mashindano ya CAF ilikuwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya makundi iliyozikutanisha Al Hilal ya Sudan na MC Alger ya Algeria, Novemba 21, 2025 katika Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.

Katika mchezo huo, Al Hilal iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya MC Alger.

Jumapili Septemba 6, 2026, Bulu atashika filimbi kwa mara nyingine tena katika uwanja wa taifa wa Bingu huko jijini Lilongwe ambapo wenyeji Mighty Wanderers watavaana na Simba.

Katika mchezo huo, Bulu atasaidiwa na waamuzi wenzake raia wa Ghana, Seth Abletor na Richard Kweku Nartey, ambao watakuwa waamuzi wasaidizi, huku Grema Mohammed wa Nigeria akiwa mwamuzi wa nne.


KUANGUKA UWANJANI

Moja ya tukio la huzuni kwa Bulu lilitokea Machi 30, 2021, wakati alipokuwa akichezesha mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) kati ya Ivory Coast na Ethiopia jijini Abidjan.

Katika dakika za mwisho za mchezo, joto kali na changamoto ya upungufu wa maji mwilini vilimfanya mwamuzi huyo kuonekana akiyumba kabla ya kuanguka uwanjani.

Madaktari waliingia haraka kumhudumia kabla ya kutolewa uwanjani na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

Tukio hilo halikumzuia kuendelea na kazi yake ya uamuzi, badala yake aliendelea kupata uteuzi katika mashindano tofauti ya soka barani Afrika.