Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simbu ajitosa kuibua vipaji

SIMBU Pict

Muktasari:

  • Simbu ana kumbukumbu nzuri ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka huu 2025 kwenye mbio za Boston Marathon za Marekani akitumia muda wa 2:05:04.

MWANARIADHA wa Kimataifa wa Tanzania, Alphonce Simbu amejitosa kuibua vipaji vya michezo lengo ikiwa ni kuwa daraja la vijana kutimiza ndoto zao kama ilivyo kwake.

Simbu ana kumbukumbu nzuri ya kumaliza katika nafasi ya pili mwaka huu 2025 kwenye mbio za Boston Marathon za Marekani akitumia muda wa 2:05:04.

Hiyo ilimfanya kuwa Mtanzania wa nne kumaliza ndani ya nafasi mbili za juu katika mbio hizo, wengine wakiwa ni Gabriel Geay mwaka 2023, Juma Ikangaa mwaka 1988 na 1989 akimaliza nafasi ya pili mara zote nyuma ya bingwa wa Kenya, Ibrahim Hussein ambaye kwa sasa ni mkufunzi na msimamizi wa kituo cha usimamizi wa michezo ya riadha kanda ya mashariki.

Mwenye rekodi hiyo pia ni mwanariadha Boay Akonaay ambaye naye alishika nafasi hiyo hiyo ya pili mwaka 1995 katika mbio hizo zinazoandaliwa na Benki Kuu ya Marekani zikiwa na umaarufu mkubwa sana.

Sasa ameonyesha dhamira ya kuibua vipaji kupitia tamasha la michezo la Mampando ambalo lilifanyika wilayani Ikungi Mkoa wa Singida kwa kuandaliwa na taasisi ya Alphonce Simbu Foundation lililoshirikisha michezo mbalimbali ikiwamo mpira wa miguu na riadha.

Simbu alisema kama mwanariadha anatamani sana kuona vijana wa vijijini nao wanatimiza ndoto zao kupitia michezo kama ilivyo kwake kwa upande wa riadha ndio maana amekuwa akipambania hili kuwashika mkono na kuwafanya wafikie malengo yao.

“Nafurahi kuona kupitia tamasha la Mampando kuna vijana wengi hasa kwa upande wa riadha wamepata nafasi ya kuchaguliwa na makocha na sasa wako jijini Arusha wanafanya mazoezi.

“Kwangu mimi naamini miaka inayokuja watatokea nyota wengine wazuri zaidi yangu ambao wataendelea kuipambania nchi yetu,” alisema Simbu.

Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Wakili Jackson Ndaweka alisema wanashirikiana na Simbu kuhakikisha vipaji vingi vinaibuliwa kupitia tamasha la Mampando ambayo itatoa nafasi kwa vijana kuweza kutimiza ndoto zao.

“Vipaji vya watu kama kina Simbu ukiangalia chimbuko lao ni watu ambao wametokea shuleni na mchezaji ambaye anakuwa katika levo ya shule anakuwa mikononi mwa wazazi.

“Kama RT kikubwa ambacho tunaweza kufanya kwa vijana wadogo kama hawa ni kutoa mafunzo kwa walimu katika shule ambazo wanasoma ndio maana tumekuwa tukiendeleza kozi ya Kids Athletics, lengo ni kuwapa uelewa wa mchezo wa riadha unavyoenda,” alisema Ndaweka.

Angelina John, mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania alisema kuna haja ya serikali kuandaa mbio mbalimbali za viwanjani kwa upande wa shuleni.


Naye Rogath John, Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha (ARAA), aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya vijana ambao wakionyesha vipaji vikubwa sana ambapo wameanza mchakato wa kuwasiliana na wazazi wao kuona namna gani watawachukua hili kwenda kuwaendeleza kupitia mchezo wa riadha.