Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yatozwa faini

Muktasari:

KLABU ya Simba imetozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la washabiki wake kurusha chupa tupu na zenye maji uwanjani na kusababisha mchezo wake dhidi ya Gwambina kusimama kwa zaidi ya dakika tatu hadi polisi walipoingilia kati kutuliza ghasia hiyo.

KLABU ya Simba imetozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la washabiki wake kurusha chupa tupu na zenye maji uwanjani na kusababisha mchezo wake dhidi ya Gwambina kusimama kwa zaidi ya dakika tatu hadi polisi walipoingilia kati kutuliza ghasia hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Aprili 28, 2021 imesema kuwa adhabu hiyo imetolewa baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kukaa kikao chake cha Aprili 27, 2021 cha kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili.

“Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 45(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu” imesema  taarifa hiyo

Tukio hilo lilitokea katika mchezo uliochezwa Aprili 24, 2021 kwenye uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Katika mchezo huo, mchezo ulisimama kwa muda baada mashabiki wa Simba kumrushia chupa za maji mwamuzi wa pembeni, Geoffrey Msakila baada ya kunyoosha kibendera kulikataa bao lililofungwa na Joash Onyango akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Clatous Chama.