Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaatangaza uzi mpya kimataifa

Simba yaatangaza uzi mpya kimataifa

Muktasari:

  • Klabu ya Simba imetangaza jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020/21

KLABU ya Simba imetangaza jezi mpya watakazotumia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wao wanaanzia ugenini kucheza na Plateau United ya Nigeria.

Simba itacheza mechi hiyo Novemba 27 mwaka huu na mechi ya marudiano itachezwa jijini Dar es Salaam huku wakiweka wazi jezi zao za nyumbani na ugenini.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo Dewji' alisema uongozi utaanza kutangaza mambo mbalimbali yanayofanywa kwenye klabu yao kuanzia wiki hii.

Jambo la kwanza kutangaza ni jezi mpya ambazo zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali nchini.

Mbali na jezi hizo, pia Mo alisema hata usajili wa wachezaji wao waliowaongeza mikataba utaanza kutangazwa kupitia mitandao yao ya kijamii kama walivyofanya jioni ya leo Jumatano walipotangaza jezi hizo.

_________________________________________________________

MWANDISHI WETU