Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Queens yaendeleza ubabe

SIMBA Q Pict

Muktasari:

  • Simba imeanza vizuri msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate Princess katika mchezo uliopigwa Novemba 4, 2026, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

KOCHA wa Simba Queens, Mussa Hassan ‘Mgosi’, amesema licha ya timu yake kupata pointi tatu dhidi ya Fountain Gate Princess, michezo baina yao imekuwa na ushindani mkubwa kutokana na ubora wa timu zote mbili.

Simba imeanza vizuri msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate Princess katika mchezo uliopigwa Novemba 4, 2026, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha ushindi wa mechi mbili mfululizo, baada ya kuanza kampeni zake kwa kuichapa Kilimanjaro Wonders mabao 3-0.

SIMB 01
SIMB 01

Akizungumzia mchezo huo, Mgosi amesema mechi dhidi ya Fountain Gate zimekuwa ngumu licha ya Simba kuendelea kupata matokeo mazuri kila zinapokutana na timu hiyo.

“Mechi zote ambazo tunacheza na Fountain Gate hazijawahi kuwa rahisi. Tunapata pointi tatu lakini zinakuwa ngumu. Tunaamini pia mechi ya marudiano itakuwa ngumu zaidi,”amesema.

Kocha huyo ameongeza kuwa hata timu nyingine zinapokutana na Simba huingia uwanjani zikiwa na dhamira ya kutoa ushindani mkubwa kwa sababu zinaitambua kama mojawapo ya timu bora katika ligi hiyo.

SIMB 02

Hata hivyo, ushindi huo umeendeleza rekodi nzuri ya Simba Queens dhidi ya Fountain Gate Princess, ambao katika michezo 12 iliyopita, Simba ilikuwa ikipata pointi zote tatu kila ilipokutana na mpinzani huyo.

Kwa ushindi wa bao 1-0, Simba imefikisha ushindi wa 13 dhidi ya Fountain Gate katika michezo baina yao. Hii ina maana kuwa katika mechi zote 13 zilizochezwa, Fountain Gate haijapata ushindi wala sare dhidi ya Simba Queens.