Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sichone afunguka sababu ya kurejea Bongo

Muktasari:

  • Sichone alijiunga na Gulf United akitokea Trident FC ya Zambia, ambako alifanya vizuri kwa akicheza mechi 18, alifunga mabao sita na kutoa asisti nane.

BAADA ya kuitumikia Gulf United ya Falme za Kiarabu kwa msimu mmoja, mshambuliaji wa Tanzania, Morice Sichone amerejea Tanzania na kusaini mkataba wa miaka miwili katika kikosi cha Pamba Jiji.

Sichone alijiunga na Gulf United akitokea Trident FC ya Zambia, ambako alifanya vizuri kwa akicheza mechi 18, alifunga mabao sita na kutoa asisti nane.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sichone alisema sababu ya kurejea Tanzania ni kwa ajili ya kupata utulivu zaidi wa kucheza soka.

Uamuzi huo unakuja baada ya msimu ambao pia alikumbwa na changamoto za mazingira ya kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati, hali iliyomfanya arejee Tanzania na kuangalia mazingira ya utulivu ya kuchezea soka.

“Nimeamua kurudi Tanzania kwa sababu nataka kupata utulivu. Nimecheza Gulf kwa msimu mmoja, lakini kulikuwa na changamoto za mazingira ya vita yaliyokuwa yanaendelea huko. Nikaona ni bora nirejee nyumbani na kuendelea kucheza nikiwa katika mazingira ya utulivu zaidi,” alisema Sichone.

“Lakini pia nilipitia changamoto ya kufiwa na baba yangu, hivyo nimeamua kurejea kukaa karibu na mama ili kuendelea kumfariji na asiwe na wasiwasi kubwa kuhusu mimi.”

Akiwa Gulf mshambuliaji huyo alifunga mabao matano katika mechi nane alizocheza.Inaelezwa Pamba Jiji imemsajili ili kuongeza ushindani kwenye safu ya ushambuliaji.

Ujio wake unatajwa kwend kuziba pengo la Mkenya, Tegis Momanyi ambaye alikuwa mshambuliaji kinara wa timu hiyo alipofunga mabao 11 ya Ligi Kuu.