Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jammy anukia Misri

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyeifungia KMC bao katika Ligi Kuu Bara 2025-2026, yupo katika hatua nzuri za kujiunga na Petrojet, huku Petrol Asyout ya Misri pia kuonyesha uhitaji wa saini yake.

MSHAMBULIAJI Jammy Simba yuko katika hatua nzuri za kujiunga na Petrojet ya Misri baada ya kufikia makubaliano ya awali kutokana na kuonyesha kiwango cha kuridhisha akiwa KMC msimu wa 2025-2026, licha ya timu hiyo kushuka daraja.

Nyota huyo aliyeifungia KMC bao katika Ligi Kuu Bara 2025-2026, yupo katika hatua nzuri za kujiunga na Petrojet, huku Petrol Asyout ya Misri pia kuonyesha uhitaji wa saini yake.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo aliliambia Mwanaspoti kwamba makubaliano ya awali yamefikiwa na sasa ni mambo madogo yaliyobakia, kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka mitatu wenye kipengele cha kuongeza mwingine mmoja.

“Kila kitu kinaenda vizuri na tunatarajia muda wowote kukamilisha uhamisho huo, Petrojet imevutiwa na kipaji chake na kufungua mazungumzo na hadi sasa yanaenda kukamilika, ni hatua nzuri kwake na taifa kwa ujumla,” kilisema chanzo hicho.

Mshambuliaji huyo aliyezaliwa Julai 15, 2006, alijiunga na KMC katika dirisha dogo la Januari 2025, akitokea JKU ya Zanzibar na kuonyesha kiwango kizuri, baada ya kupata nafasi ya kuchezea timu za taifa za vijana chini ya miaka 20.

Ikiwa uhamisho huo utakamilika atakuwa mchezaji wa pili hivi karibuni kutoka KMC kusajiliwa Misri baada ya beki Rahim Shomary kujiunga na Ghazl El Mahalla Julai 14, 2025. Alirejea nchini  Januari 26, 2026 na kujiunga na Singida Black Stars.