Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KVZ bingwa mara sita mfululizo netiboli Zanzibar

Muktasari:

  • KVZ ilimaliza ligi hiyo ikiwa na pointi 10 baada ya kushinda michezo yote mitano iliyocheza ikifunga magoli 306 na kufungwa 136 jambo lililoonesha ubora wao.

TIMU ya KVZ imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Netiboli Zanzibar kwa mara ya sita mfululizo baada ya kumaliza kinara katika msimamo wa Ligi hiyo.

KVZ ilimaliza ligi hiyo ikiwa na pointi 10 baada ya kushinda michezo yote mitano iliyocheza ikifunga magoli 306 na kufungwa 136 jambo lililoonesha ubora wao.

Nafasi ya pili ya ligi hiyo imechukuliwa na Zimamoto ambayo ilifanikiwa kukusanya pointi nane kwa kushinda michezo minne na kupoteza mmoja ambapo ilifunga magoli 349 na kufungwa 137.

Timu ya JKU imemaliza ya tatu ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mchezo mmoja na kupoteza minne huku Mafunzo ikimaliza ya nne na pointi nne.

Kwa upande wa Bandari, imemaliza nafasi ya tano ya msimamo wa Ligi hiyo kwa kuwa na pointi nne na Nungwi imemaliza nafasi ya mwisho baada ya kufungwa magoli 314 na kufunga 38.

Katika mchezo wa mwisho, KVZ iliibuka na ushindi wa magoli 43-32 dhidi ya JKU katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Gymkhana, Unguja.

KVZ ilianza vizuri mchezo huo na kumaliza robo ya kwanza ikiwa mbele kwa 11-8 kabla ya kuongeza kasi katika robo ya pili na kuongoza kwa 26-15.

Katika robo ya tatu, KVZ iliendelea kutawala mchezo na kufikisha 33-25 dhidi ya JKU, kabla ya kuhitimisha mchezo kwa ushindi wa 43-32.

Katika mchezo mwingine uliochezwa mapema saa 8:00 mchana, Bandari iliifunga Nungwi 36-14.