Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shalulile aitwa Brave Warrious mechi za kufuzu AFCON 2027

Muktasari:

  • Shalulile, ambaye alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ni miongoni mwa washambuliaji 11 waliotajwa na kocha mkuu.

Mshambuliaji wa Yanga, Peter Shalulile, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Namibia, Brave Warriors, kitakachoshiriki mechi za kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2027.

Orodha hiyo ina jumla ya wachezaji 29, huku Shalulile akiwa miongoni mwa majina makubwa kwenye safu ya ushambuliaji.

Shalulile, ambaye alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ni miongoni mwa washambuliaji 11 waliotajwa na kocha mkuu, Collin Benjamin katika kikosi hicho.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa, Shalulile atakuwa miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuiongoza Namibia katika kampeni za kufuzu AFCON 2027.

Kuitwa kwa Shalulile kunakuja ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa yeye kuwa mchezaji muhimu wa taifa hilo, akiwa pia nahodha wa Brave Warriors.

Mshambuliaji huyo mwenye uzoefu mkubwa katika soka la Afrika alimaliza kipindi chake cha miaka sita Mamelodi Sundowns kabla ya kujiunga na Yanga Julai mwaka huu.

Akiwa Sundowns, alifunga mabao 136 katika mashindano yote, huku pia akisaidia klabu hiyo kutwaa mataji mbalimbali, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Kikosi kamili cha Namibia kinaundwa na Mervin Kasetura (African Stars FC),Ndisiro Kamaijanda (Highbury FC), Jonas Mateus( Ongos FC), Charles Hambira ( African Stars FC), Kennedy EiB( Simba Bhora),Riaan Hanamub (AmaZulu),Paulus Amutenya (Gaborone United), Tyrese Hikupembe (Chicken Inn), Ngero Katua (Highbury FC), Okeri Nguarambuka( African Stars FC), Alex Mumbango( Chicken Inn) naIvan Kamberipa anayecheza Gaborone United.

Wengine ni  Tully Nashixwa (Richards Bay), Approcious Petrus (Al Hilal), Ben Namib (Khomas Nampol FC), Shidolo Moses (Scottland), Sergio Damaseb (Simba Bhora) na Prins Tjiueza wa Cape Town City.

Pia kuna Shalulile kutoka Yanga, Junior Petrus( Simba Bhora), Wendell Rudath( Bucks Buccaneers), Bethuel Muzeu( Sekhukhune United), Mashiku Muyeka (Venda FC), Stoffel Witbeen ( Scottland FC), Micheal Jonas( Chula Chula), Nestor Iiyambo ( Unam FC), Deon Hotto( Orlando Pirates), David Ndeunyema (MWOS) na  Johannes Shiyave kutoka Chula Chula.

Katika kuwania kufuzu, Namibia imepangwa kundi G pamoja na Cameroon,Comoro na Congo.

Ratiba ya mechi za kufuzu imepangwa kuchezwa kwa vipindi vitatu vya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa( FIFA).

Mechi za raundi ya kwanza na ya pili zitapigwa kati ya Septemba 21  na Oktoba 6 mwaka huu.