Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hili ndiyo chama jipya la Kante

Muktasari:

  • JS El Biar ni timu mpya katika Ligi Kuu ya Algeria (Ligue 1), iliyomsajili nyota huyo baada ya awali dili lake la kwenda JS Kabylie ya Algeria pia kushindikana, jambo lililosababisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.

BAADA ya Simba kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kiungo  raia wa Senegal, Alassane Maodo Kante, kwa sasa nyota huyo amejiunga na Klabu ya JS El Biar iliyopanda daraja msimu huu kushiriki Ligi Kuu ya Algeria.


JS El Biar ni timu mpya katika Ligi Kuu ya Algeria (Ligue 1), iliyomsajili nyota huyo baada ya awali dili lake la kwenda JS Kabylie ya Algeria pia kushindikana, jambo lililosababisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.

Nyota huyo aliyejiunga na Simba, Julai 23, 2025, akitokea CA Bizertin ya Tunisia, alibakisha mkataba wa mwaka mmoja na kikosi hicho, lakini ulisitishwa kutokana na kikosi hicho kufikia idadi ya wachezaji 12 wa kigeni wanaohitajika kikanuni. Kiungo huyo aliyezaliwa Desemba 20, 2000, katika Mji wa Ziguinchor, uliopo kwao Senegal, kabla ya kuichezea CA Bizertin ya Tunisia na Simba ya Tanzania, alicheza timu mbalimbali za Senegal zikiwemo OD Ziguinchor na Union Sportive Goree.

Katika kipindi cha msimu mmoja alichoitumikia Simba, kiungo huyo alichangia mabao mawili ya Ligi Kuu Bara, japo kutokana na ushindani wa nafasi na nyota wenzake wakiwemo Yusuph Kagoma, Kelvin Nashon na Ibraheem Jabaar kumemwondoa kikosini.

JS El Biar ambayo kwa jina kamili ni Jeunesse Sportive d’El Biar, ni klabu ya soka kutoka El Biar, Algiers, huko Algeria, iliyoanzishwa Desemba 15, 1944, ikiwa ni sehemu ya historia ya soka la Algeria kwa zaidi ya miaka 81 hadi sasa. Timu hiyo iliandika historia mpya Aprili 10, 2026, baada ya kupanda daraja kutoka Ligue 2 hadi Ligue 1 ambayo ni Ligi Kuu ya Algeria, huku ikiamini uzoefu wa Kante ni chachu pia ya kikosi hicho kufikia malengo ya kufanya vizuri msimu huu.