Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shabiki Chelsea asomba 122 milioni

Ghafla shabiki mmoja wa Chelsea Nurdin Abdallah mkazi wa Kigogo amejikuta milionea baada ya kutusua mkwanja wa Sh 122 milioni kupitia ubashiri wa Premier Bet.

Abdallah ambaye hakuwahi kushinda kiasi kikubwa kama hicho katika simulizi yake amesema licha ya kuwa ni shabiki wa Chelsea lakini hakuweza kuitabiria timu yake hiyo matokeo.

Abdallah amesema mbali na Chelsea alizikimbia timu zingine kubwa kwenye ligi ya England akihofia kujiharibia ubashiri wake kutokana na matokeo yao ya hivi karibuni.

"Sikuzitaka hizo timu kubwa nilizikimbia nilichagua timu kama sita tu na kwenye hizo timu kubwa ilikuwa Tottenham na nikashinda ,unajua hizi timu kubwa kwasasa hazina matokeo mazuri,"amesema Abdallah

Aidha Abdallah ameongeza kuwa kwa kuwa anajihusisha na kazi ya kuuza vitu vya elektroniki anataka Sasa kwenda kuzitumia fedha hizo kutanua biashara zake.

"Mimi Sasa nataka niwe nakwenda hata nje ya nchini hata China kuchukua vitu ili nijiendeleze biashara yangu tofauti na Sasa nikitumia fedha hizi."

Kwa upande wa Afisa Masoko wa kampuni hiyo Erick Kirita amesema baada ya ushindi huo wa Abdallah watahakikisha wanamsadia mshindi huyo kumpatia ushauri wa kibiashara kupitia anachotaka kukifanya ili kuweza kujenga Taifa.

"Jamii inatakiwa kufahamu kwamba hatutaki watu wacheze michezo ya kubashiri kama kazi ya kuwaingizia kipato tunataka watumie kama michezo mingine lakini kwetu hapa huwa mshindi akipata fedha nyingi tunamsaidia kumtafutia washauri wa kibiashara ili aweze kwenda kuwa na muongozo mzuri wa kile anachotaka kufanya,"amesema Kirita