Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali kuzipiga tafu KVZ, KMKM kimataifa

KMKM Pict

Muktasari:

  • Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo Agosti 18, 2026 kwenye Uwanja wa Mao Zedong kisiwani Unguja wakati wa sherehe za KVZ Day.

NAIBU Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein, amesema KVZ na KMKM zina jukumu kubwa la kuiwakilisha Zanzibar katika mashindano ya kimataifa, hivyo Serikali itaziunga mkono ili kujiandaa kupata matokeo mazuri.

Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo Agosti 18, 2026 kwenye Uwanja wa Mao Zedong kisiwani Unguja wakati wa sherehe za KVZ Day.

Katika kufanikisha hilo, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika kwa KVZ na KMKM katika maandalizi yao kuelekea mashindano hayo.

“Serikali itaendelea kushirikiana na timu ya KVZ na KMKM kuhakikisha zinajiandaa vizuri katika mashindano hayo ya klabu bingwa na Shirikisho la Afrika,” amesema.

Pia, aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu, kujituma na kutumia vipaji vyao kucheza soka zuri ili kupata matokeo yatakayoinua heshima ya Zanzibar kupitia michezo.

Naye Mkuu wa kikosi cha KVZ, Said Ali Shamhuna, amesema ushiriki wa timu hiyo kimataifa ni fursa kubwa ya kuitangaza Zanzibar, hivyo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wanakaa pamoja kuandaa mikakati ya kuitengeneza timu imara.

Mechi za hatua ya awali ya michuano ya CAF zimepangwa kuchezwa kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu ambapo KVZ katika Ligi ya Mabingwa Afrika, itaanzia ugenini kucheza dhidi ya Swehly SC ya Libya, kisha kurudiana kati ya Septemba 11 na 13, 2026.

Kwa upande wa KMKM inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika, pia itaanzia ugenini kuikabili Al Ahli Tripoli ya Libya, itamalizia nyumbani.