Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam, Singida BS zitazidi kukomaa kimataifa

AZAM Pict

Muktasari:

  • Kuna timu nyingi nzuri na zenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa ambayo zilitegemewa zingekuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini zimeangukia katika Kombe la Shirikisho Afrika.

MSIMU huu Kombe la Shirikisho Afrika limejaza wababe wengi sana na mashindano hayo yanaonekana hayatokuwa mepesi.

Kuna timu nyingi nzuri na zenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa ambayo zilitegemewa zingekuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini zimeangukia katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Hapana shaka, timu tishio zaidi kwenye mashindano hayo msimu huu ambayo hapa kijiweni wote tumekubaliana ni miamba ya Misri, Al Ahly ambayo baada ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika kwa muda mrefu, sasa wameangukia Kombe la Shirikisho.

Al Ahly wametwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mara moja lakini wamechukua Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika mara 12.

Wababe wengine ni Raja Casablanca ya Morocco ambayo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu yao msimu uliomalizika, wameangukia Kombe la Shirikisho msimu huu.

Hao pia ni mfano wa timu zenye mafanikio makubwa zaidi Afrika ambazo zitakuwepo katika Kombe la Shirikisho msimu ujao kwani wametwaa taji hilo mara mbili na wamechukua Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu.

Hata hivyo, pamoja na uwepo wa klabu hizo na nyinginezo zenye majina makubwa, wawakilishi wetu wa Tanzania katika mashindano hayo, Azam FC, Singida Black Stars na KMKM hawapaswi kuyacheza kwa woga.

Wachukulie uwepo wa klabu tishio katika hayo mashindano kwa mtazamo chanya ambao utazisaidia kuimarika na kuwa bora zaidi na kuongeza uzoefu wa mashindano ya kimataifa.

Msimu uliopita, Singida Black Stars na Azam FC ziliweza kuingia hatua ya makundi kwenye mashindano hayo hivyo hazitakiwi kuendelea kujiona ni timu ndogo.