Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Selemani Mwalimu amaliza utata Simba

Muktasari:

  • Mwalimu, ambaye msimu uliopita aliitumikia Simba kwa mkopo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco, amekuwa kwenye sintofahamu baada ya klabu hizo mbili kutofautiana kuhusu makubaliano ya kuendelea kwa mshambuliaji huyo kubaki Msimbazi.

MSHAMBULIAJI Selemani Mwalimu, amewaondoa hofu mashabiki wa Simba kuhusu hatma yake baada ya video yake kuonyeshwa kwenye skrini iliyowekwa Uwanja wa Uhuru wakati wa kilele cha Simba Day, akithibitisha kuwa ataendelea kuwepo msimu wa 2026-2027.

Mwalimu, ambaye msimu uliopita aliitumikia Simba kwa mkopo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco, amekuwa kwenye sintofahamu baada ya klabu hizo mbili kutofautiana kuhusu makubaliano ya kuendelea kwa mshambuliaji huyo kubaki Msimbazi.

Baada ya msimu wa 2025-2026 kumalizika, Simba ilitangaza kuwa imefikia makubaliano ya kuendelea na Mwalimu, lakini Wydad baadaye ilikanusha taarifa hizo.

Katika kipindi hicho, Mwalimu alirejea Morocco na kuonekana akifanya mazoezi na Wydad, jambo lililozua maswali kuhusu iwapo angebaki Casablanca au kurejea Tanzania.

Akizungumza kupitia video hiyo, Mwalimu aliwatumia ujumbe mashabiki wa Simba na kuthibitisha kuwa bado ni sehemu ya kikosi hicho.

“Nipende kuwapa hongera Wanasimba wote. Nitakuwepo msimu huu, ni mchezaji halali. Niwape habari Wanasimba wote na niwatakie heri miaka 90 ya Simba,” amesema Mwalimu.

Hata hivyo, baadae Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alitolea ufafanuzi na kueleza kilichokuwa kinaendelea kuhusu mchakato wa kumrejesha Mwalimu kutoka Wydad.

“Mmeamini mtoto bado ni mali ya Simba na muda huu yupo njiani Casablanca anarudi nyumbani, wamekwenda kupeleka majungu Morocco na mwisho wa siku Mwalimu amechagua kubaki Simba na Wydad imekubali kufanya biashara na Simba,” amesema Ally.