Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Simba achomolewa kikosini kiaina

Muktasari:

  • Katika ujumla ya  wachezaji nyota 31  waliotambulishwa kwenye tamasha la Simba Day kwa ajili ya msimu wa 2026-2027, jina la Kante halikutajwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, licha ya kukiri bado ni mali yao na watatoa taarifa zake.

KIUNGO Alassane Kante amechomolewa kiana ndani ya Simba baada ya  kutotangazwa kwa ajili ya kukitumikia kikosi hicho msimu wa 2026-2027.

Katika ujumla ya  wachezaji nyota 31  waliotambulishwa kwenye tamasha la Simba Day kwa ajili ya msimu wa 2026-2027, jina la Kante halikutajwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, licha ya kukiri bado ni mali yao na watatoa taarifa zake.

"Naomba niseme jambo moja kuhusu Kante, bado ni mchezaji wetu na taarifa zake tutazitoa baadae," amesema Ahmed Ally.

Hata hivyo, Mwanaspoti linatambua kuna uwezekano mkubwa kwa nyota huyo akauzwa moja kwa moja, kwani hadi sasa kikosi hicho tayari kina wachezani 12 wa kigeni waliotambulishwa leo kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano tofauti.

Nyota huyo raia wa Senegal alijiunga na Simba, Julai 23, 2025, baada ya kuachana na CA Bizertin ya Tunisia, japo maisha yake ndani ya kikosi hicho yamekuwa magumu kutokana na ushindani uliopo na nyota wengine.