Sasii avalishwa beji ya FIFA
MWAMUZI aliyeipatia Simba penalti ya utata katika mechi yao na KMC uliomalizika kwa Simba kushinda bao 1-0, Hery Sasii ni miongoni mwa waamuzi 17 walioteuliwa kuvaa beji za Shirikisho la Soka la kimataifa (FIFA) mwakani.
Taarifa ya waamuzi hao imetolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuwataja wengine kwa waamuzi wa kati kuwa ni Florentina Zablon, Jonesia Rukyaa, Martin Saanya, Mfaume Nassoro na Ramadhan Kayoko.
Waamuzi wasaidizi ni Abdulaziz Ally, Ferdinand Chacha, Frank Komba, Hellen Mduma, Janet Balama, Kassim Mpanga, Mbaraka Haule, Mohamed Mkono na Soud Lila.
"Katika soka la ufukweni waamuzi walioteuliwa na Geofrey Tumaini na Jackson Msilombo," imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa leo Ijumaa, Desemba 18, 2020.