Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruvu kutambulisha nane wapya

KLABU ya Ruvu Shooting imejitapa kesho kutangaza wanajeshi wake 25 watakao ingia kambini kujiweka sawa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Ruvu walimaliza nafasi ya 11 katika msimu uliomalizika wakiwa na alama 41 wamesema katika wachezaji watakao watambulisha kutakuwa na maingizo mapya nane ili kuimarisha kikosi chao.

Akizungumza ma Mwanaspoti Afisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire anasema baada ya klabu yao kukamilisha usajili wa msimu 2021/2022 kesho watataja majina ya wachezaji wote watakao kuwa nao kueleke msimu huo.

"Suala la usajili kulingana na maitaji ya kocha umekamilika na tunategemea kesho kutangaza kikosi chetu na lini wataingia kambini rasmi kujianda na msimu", amesema Masau.


Imeandikwa na Lilian Mukulu