Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Robertinho, Nabi ni ufundi na mbinu

Muktasari:

  • Namna makocha hao watakavyoviandaa vikosi vya kimbinu pamoja na jinsi watakavyovipanga kutegemeana na tathimin ambayo kila imefanya juu ya ubora na udhaifu wake pamoja na ule wa mpinzani inaonekana itaamua mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

MAKOCHA Nasreddine Nabi na Roberto Oliviera 'Robertinho' wameshikilia funguo za ushindi kwa timu zao katika mechi itakayozikutanisha leo Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni.

Namna makocha hao watakavyoviandaa vikosi vya kimbinu pamoja na jinsi watakavyovipanga kutegemeana na tathimin ambayo kila imefanya juu ya ubora na udhaifu wake pamoja na ule wa mpinzani inaonekana itaamua mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

Wamekuwa na baadhi ya mambo ambayo wanafanana katika uchezaji wa timu zao hasa kumiliki mpira lakini wamekuwa wakitofautiana katika mambo mengine.
Wote wamekuwa wakitegemea eneo la kiungo kama uti wa mgongo katika kuzalisha mashambulizi, kuilinda timu na kutengeneza balansi ya mchezo.


Robertinho
Ni mmoja wa makocha ambao wanaoamini katika soka la kushambulia kwa haraka pindi timu inapopata mpira na anapendelea kuona kundi kubwa la wachezaji linafanya hivyo.
Mfumo ambao amekuwa akiutumia katika mechi nyingi za Simba ni ule wa kawaida wa 4-2-3-1 lakini kuna nyakati kadhaa huwa anatumia ule wa 4-4-2.
Pindi Simba inapokuwa na mpira, kocha huyo amekuwa akipendelea kuona ikishambulia kwa haraka na kundi kubwa la wachezaji lishiriki katika kutengeneza mashambulizi na hata kufunga mabao.
Sio kocha ambaye amekuwa akitumia zaidi mawinga kucheza nyuma ya mshambuliaji na badala yake anapendelea kuwapanga zaidi viungo washambuliaji kwa lengo la kuhakikisha wanampa huduma za kutosha straika wake.
Pindi Simba inapokuwa haina mpira, Robertinho anapendelea kuona kila mchezaji akishiriki katika kuusaka kutoka kwa timu pinzani hasa wale wa nafasi za ushambuliaji ambao amekuwa akipenda kuona wanaweka msukumo mkubwa kwa walinzi wa timu pinzani ili kuwanyima uhuru wa kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma.
Ni kocha anayependa kuona timu yake  ikicheza soka la moja kwa moja (direct gootball) akiamini ni njia sahihi ya kujiweka katika uwezekano mkubwa wa kupata ushindi lakini pia hapendelei kuona mchezaji wake akikaa muda mrefu na mpira mguuni.
Bahati mbaya ni kwamba hili litakuwa pambano la kwanza la Kariakoo Derby kwa Robertinho, licha ya uzoefu alionao kwenye mechi za aina tangu akiwa Rwanda, Angola na Uganda, lakini bado kocha huyo anaweza kutumia nafasi hiyo ya kutozoeleka kwenye derby kuiduiwaza Yanga.


Nasreddine Nabi
Kocha Nabi amekuwa akipendelea zaidi kutumia mfumo wa 4-2-3-1 ingawa kuna nyakati huipanga timu yake kucheza ule wa 4-3-3.
Wachezaji watatu ambao wanacheza nyuma ya mshambuliaji wa kati, Nabi huwatumia mawinga wawili na kiungo mmoja wa kushambulia.
Mara nyingi Nabi amekuwa akipendelea kuona mawinga hao pindi wanapokuwa na mpira kukatiza kwa kuelekea katika lango la timu pinzani kwa ajili ya kutengeneza nafasi au kufunga bao badala ya kukimbilia pembeni kupiga krosi.
Winga ambaye amekuwa akitumika kushambulia sana ni yule wa upande wa kulia wakati wa upande wa kushoto mara kwa mara huongeza namba ya wachezaji karibu na eneo la hatari la timu pinzani ili kutoa mwanya kwa Joyce Lomalisa kupiga krosi.
Injini ya timu ni kiungo Khalid Aucho ambaye ndiye amekuwa akiiendesha Yanga kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi sahihi hasa zile za kuelekea mbele na maamuzi yake ya haraka pindi awapo na mpira yamekuwa silaha yake kuvunja mipango ya timu pinzani.
Aucho amekuwa akinufaika sana na uwepo wa Yannick Bangala anayecheza naye sambamba katika nafasi ya kuilinda safu ya ulinzi pinzani hasa katika kupora mipira na kutibua mashambulizi ya wapinzani.
Nabi ni muumini wa soka la pasi fupifupi za taratibu pindi timu yake inapokuwa na umiliki wa mpira.