Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pwani, Dar zilivyochuana mashindano ya riadha

Salma Charles na Zainab Issa (Kulia) wakichuana katika mbio za mita 800 kwenye mashindano ya Ujirani Mwema hivi karibuni kwenye viwanja vya Filbert Bayi Kibaha.

Wanariadha wa Dar es Salaam na wale wa Pwani wamegawana ushindi kwenye mashindano ya Ujirani mwema yaliyofanyika kwa mara ya kwanza kwenye viwanja vya Filbert Bayi Kibaha mkoani Pwani.

Mashindano hayo yaliyolenga kuibua na kuendeleza vipaji vya riadha kwenye mikoa mitatu ya Morogoro, Dar es Salaam na Pwani yalishirikisha wakimbiaji 60 kutoka mikoa miwili.

"Wenzetu wa Morogoro wamepata changamoto na kushindwa kuja, tutakuwa nao kwenye mashindano yajayo," amesema katibu wa riadha mkoa wa Pwani Robert Kalyahe.

Amesema, mashindano hayo yatakuwa yakifanyika mara kwa mara yakilenga kuimarisha na kuboresha vipaji vya wanariadha wa mikoa hiyo kwenye mbio za uwanjani (mita 100 hadi 10000) na michezo ya miruko na mitupo.

Awali, mlezi wa riadha mkoa wa Pwani aliyekuwa mdhamini wa mashindano hayo, Filbert Bayi aliwasisitiza wanariadha walioshiriki mara ya kwanza kuendelea kushiriki kwani muda wao unarekodiwa kuona kama kuna maboresho au vinginevyo.

"Hata kama ulikimbia time (muda) mbaya leo (juzi), una nafasi ya kuboresha muda wako na kufanya vizuri, msiache kuchuana mara zote mashindano hayo yanapofanyika hii itawaaidia kuboresha time zenu," amesema Bayi.

Katika mashindano hayo, timu ya Dar es Salaam iling'ara kwa kushinda nafasi ya kwanza hadi ya tatu kwenye mbio ya mita 1500 ya wanaume.

Emmanuel Josephat alikuwa mshindi akitumia dakika 4:35:25, Modest Nathamel alimaliza wa pili kwa dakika 4:57:31 na Florian Boniface aliyekimbia dakika 5:01:67 alikuwa wa tatu.

Wakati kwa wanawake, Sara Masalu alikuwa kinara kwa dakika 5:07:41 akifuatiwa na Zainabu Issa (5:09:28) na Salma Charles (5:14:95) wote wa Pwani.

Salma tena alishinda mbio ya mita 800 akitumia dakika 2:25:53 akifuatiwa na Sarah (2:26":47) na Sharifa Mawazo alimaliza wa tatu kwa dakika 2:29:30 wote kutoka Pwani.

Kwa wanaume, Rajabu Athumani a Pwani alikuwa kinara akitumia dakika 2:18:56 akifuatiwa na Mathayo Jeremia (2:21:34) na Florian Boniface aliyekimbi dkika 2:25:17 alihitimisha tatu bor wote kutoka Dar es Salaam.

Pwani ilitakata kwenye mbio ya mita 200 wanawake, wanariadha Siwema Julius (sekunde 28.62), Shija Donald (sekunde 29.43) na Coletha Anthony (sekunde 31.91) walikamata nafasi ya kwanza hadi ya tatu.

Kwenye mbio ya mita 400 kwa wanaume na wanawake, Pwani ilitwaa ushindi ikiongozwa na Benedicto Mathias (sekunde 52:72), Samwel Yohana (54:34) na William John (56:08).

Wanawake ni Sharifa Mawazo  (dakika 1:04:56), Lucy Pius (1:05:78) na Meryciana Mateso (1:09:11), wakati kwenye mbio ya mita 100 ya wanaume, Emmanuel Amos alishinda akitumia sekunde 11.63, Kimane Kibase alimaliza wa pili akitumia sekunde 11.78 wote wa Pwani na Gipson Mnenei wa Dar es Salaam alimaliza wa tatu kwa sekunde 12,09.

Katibu wa Riadha mkoa wa Dar es Salaam, Samwel Mwera amesema huo ni mwanzo wa mikoa hiyo kurejesha mbio za uwanja na kumshukuru Filbert Bayi kwa kutoa zawadi pesa taslimu kwa washindi.

"Imekuwa ni sapraizi, hatukujua kama mzee wetu (Bayi) angefanya hiki kitu, lakini kuwapa vijana motisha kama hii kunaongeza ushindani, kama mikoa tutaona namna ya kujipanga ili kuendeleza jambo hili lililofanywa na mzee Bayi," amesema.

Amesema, mikoa hiyo mitatu (Dar, Pwani na Morogoro) imejikita kufufua mbio za uwanjani na michezo ya miruko na mitupo nchini.

"Wenzetu Kaskazini (mikoa ya Arusha na Moshi) wako vizuri kwenye mbio ndefu, hivyo sisi tumeamua kuiwekea mikakati mbio fupi, za kati na ndefu za uwanjani na michezo ya miruko na mitupo ili kuirejesha kwenye ramani ya riadha nchini," amesema.