Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga waanza mapema CAF, droo kupangwa Alhamisi

Muktasari:

  • Hii ina maana miamba hiyo ya Kariakoo italazimika kushuka dimbani mapema mwezi Septemba kusaka ushindi utakaowavusha kwenda hatua inayofuata, huku safari ya kuelekea hatua ya makundi ikianza mapema kuliko ilivyokuwa kwa baadhi ya vigogo wa bara hilo.

Vigogo wa soka Tanzania, Simba na Yanga, wataanza kampeni zao za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2026/27 kuanzia hatua ya kwanza ya awali, baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuthibitisha ratiba ya mashindano hayo.

Hii ina maana miamba hiyo ya Kariakoo italazimika kushuka dimbani mapema mwezi Septemba kusaka ushindi utakaowavusha kwenda hatua inayofuata, huku safari ya kuelekea hatua ya makundi ikianza mapema kuliko ilivyokuwa kwa baadhi ya vigogo wa bara hilo.

Macho sasa yataelekezwa kwenye droo ya mashindano, itakayofanyika Alhamisi, Agosti 6, 2026, katika makao makuu ya CAF jijini Cairo, Misri, ambapo Simba na Yanga watafahamu wapinzani wao wa kwanza kwenye mbio za kutafuta taji la Afrika.

Tofauti na wawakilishi hao wa Tanzania, klabu tatu pekee zimepewa nafasi ya kuanzia moja kwa moja hatua ya pili ya awali kutokana na nafasi zao za juu kwenye viwango vya ubora vya CAF.

Klabu hizo ni mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Esperance de Tunis ya Tunisia na RS Berkane ya Morocco.

Kwa Simba na Yanga, kuanzia hatua ya kwanza kunamaanisha zitalazimika kupambana kuanzia mwanzo wa safari, zikiwa na lengo la kuvuka hatua zote za mtoano na kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya ngazi ya klabu barani Afrika.