Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okwi azua gumzo Simba Day

Muktasari:

  • Katika mchezo huo uliochezwa mchana huu, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Equity, huku Okwi akifunga moja ya mabao hayo na kuwakumbusha mashabiki wa Simba makali yake yaliyowahi kuifanya kuwa kipenzi cha klabu hiyo.

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi, amezua gumzo na shangwe Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam baada ya kufunga bao katika mchezo wa kirafiki kati ya Simba Menejimenti na Equity.

Katika mchezo huo uliochezwa mchana huu, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Equity, huku Okwi akifunga moja ya mabao hayo na kuwakumbusha mashabiki wa Simba makali yake yaliyowahi kuifanya kuwa kipenzi cha klabu hiyo.

Bao hilo lilipoingia wavuni, liliibua shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki waliokuwa uwanjani, huku baadhi yao wakilitumia tukio hilo kumkumbuka mshambuliaji huyo raia wa Uganda ambaye aliwahi kuwa miongoni mwa wachezaji waliotikisa Ligi Kuu Bara akiwa na jezi ya Simba.

Okwi alijiunga na Simba kwa mara ya kwanza mwaka 2009, akitokea SC Villa ya Uganda. Alidumu Msimbazi hadi mwaka 2013 kabla ya kuondoka kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia.

Baadaye alirejea Simba mwaka 2014 kwa mkataba wa miezi sita, kabla ya kuondoka tena na kurejea mwaka 2017.

Katika kipindi chake cha kwanza Simba, Okwi alisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2011-2012.

 Baada ya kurejea mwaka 2017, aliendelea kuonyesha ubora wake wa kufumania nyavu na msimu wa 2017-2018 akafanikiwa  kumaliza akiwa mfungaji bora Ligi Kuu Bara kwa mabao 20 na kusaidia Simba kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Rekodi zinaonyesha kuwa msimu huo, Okwi alifunga mabao 20 katika mechi 28 za Ligi Kuu Bara, huku akitajwa pia kwenye kikosi bora cha msimu. Mwaka uliofuata, 2018-2019, alifunga mabao 15 katika mechi 23 za ligi na kusaidia Simba kutetea ubingwa.

Mbali na Okwi, nyota wengine waliokuwa kwenye mechi hiyo ni Meddie Kagere na John Bocco ambao nao wanabaki kuwa miongini mwa malejendi wa klabu hao.