Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MO Dewji apigwa na butwaa Ahmed Ally akiingia Uhuru na simba

MO DEWJI Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo lilitokea katika tamasha la Simba Day linalofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambapo Ally ameingia uwanjani akiwa juu ya gari lililobeba simba hao wawili, hatua iliyowafanya mashabiki kutulia kimya uwanjani wakishangaa.

MWEKEZAJI wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo Dewji’, alibaki akishangaa baada ya Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ahmed Ally, kuingia Uwanja wa Uhuru kwa staili ya aina yake akiwa na simba wawili.

Tukio hilo lilitokea katika tamasha la Simba Day linalofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambapo Ally ameingia uwanjani akiwa juu ya gari lililobeba simba hao wawili, hatua iliyowafanya mashabiki kutulia kimya uwanjani wakishangaa.

Ally alionekana kuandaa sapraizi hiyo kwa ustadi mkubwa, huku ujio wake ukiwa tofauti na ule uliozoeleka kwenye matukio ya Simba Day. 

Miongoni mwa waliokumbwa na mshangao huo alikuwa Mo Dewji, ambaye kwa muda alionekana kutazama tukio hilo kwa mshangao, kana kwamba hakuwa akiamini alichokuwa akikiona. Sapraizi hiyo iliongeza mvuto kwenye tamasha hilo lililokuwa likiendelea kwa shamrashamra mbalimbali.

MO 01

Si Mo pekee aliyeshangazwa na tukio hilo, bali pia Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alionekana kushikwa na butwaa wakati Ally akiingia uwanjani na simba hao. Kwa viongozi na mashabiki, ilikuwa ni moja ya matukio yaliyotoa picha tofauti kwenye kilele cha Simba Day.

Baada ya kuingia uwanjani na simba hao, Ally aliendelea na burudani kwa kugeukia upande wa jukwaa na kushiriki katika burudani iliyokuwa ikiendelea. 

MO 02

Simba Day ambayo huandaliwa kila mwaka na klabu ya Simba, imekuwa moja ya matukio makubwa yanayowakutanisha mashabiki wa timu hiyo kwa ajili ya utambulisho wa kikosi na burudani mbalimbali yakitumika kuongeza hamasa kabla ya msimu mpya.