Ahmed Ally alivyoteka shoo Simba Day
Muktasari:
- Ahmed Ally ameingia kwenye uwanja huo kwa staili ya kipekee akiwa amesimama juu ya kigari ambacho mara nyingi hutumiwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuweka wanyama wakali wakiwemo mbwa kwa lengo la kulinda usalama wakati wa doria.
MENEJA Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ameendelea kuteka hisia za mashabiki wa timu hiyo, baada ya kuingia kwenye Uwanja wa Uhuru kwa staili ya kipekee katika kilele cha tamasha la Simba Day.
Ahmed Ally ameingia kwenye uwanja huo kwa staili ya kipekee akiwa amesimama juu ya kigari ambacho mara nyingi hutumiwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuweka wanyama wakali wakiwemo mbwa kwa lengo la kulinda usalama wakati wa doria.
Uingiaji huo wa Ahmed Ally, umeamsha shangwe la mashabiki wa timu hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa ubunifu kwa Ofisa Habari huyo, aliyeingia kwa lengo la kuwatambulisha wachezaji wapya kwa msimu ujao wa 2026-2027.
Simba inaadhimisha kilele cha Simba Day ambacho leo kinatimiza miaka 17, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 na aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali na Makamu wake, Mwina Kaduguda 'Simba wa Yuda'.
Mbali na kuadhimisha miaka hiyo 17 tangu tamasha hilo lianzishwe, pia Simba imetimiza miaka 90 leo tangu ilipoanzishwa mwaka 1936, ikifahamika kwa jina la Sunderland.